Mwenyekiti wa Chama Cha mapinduzi CCM Wilaya ya Babati Mjini Bi Elizabeth Malley amesema kuwa chama hicho kimepata Mafanikio MAKUBWA Hususani katika uchaguzi mkuu uliopita Octoba 29.2025.
Ameyasema hayo mapema Leo Disemba 20.2025 wakati akizungumza katika mahojiano maalumu na vision media Tz mjini Babati
Ameeleza kuwa Chama hicho kimepata Mafanikio Hususani katika uchaguzi mkuu kwakufanikiwa kupata Ushindi MAKUBWA katika uchaguzi wa madiwani wabunge na Rais.
Aidha ameeleza kuwa chama hicho kilifanya kampeni za kistaarabu na kufanya kampeni za kistaarabu bila kumbugudhi mtu Wala chama Rafiki.
Vilevile ameeleza kuwa chama hicho kimefanikiwa kujenga ofisi za matawi na kata katika Wilaya hiyo.
Bi Malley ametumia fursa hiyo kuwashukuru na kuwapongeza viongozi wenzake wa Chama hicho viongozi WA serikali na wananchi Kwa ujumla na kuwaasa wananchi kudumisha Amani mshikamano na upendo ili kuendelea kufanya shughuli za maendeleo za kuliletea tija Taifa letu.
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
December 20, 2025
Rating:



No comments: