Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza linatoa taarifa kuhusu ajali iliyotokea mnamo tarehe 17 Aprili 2026 majira ya saa 2:00 usiku, katika eneo la Mihama, ndani ya maji ya Ziwa Victoria, Kata ya Kitangiri, Wilaya ya Ilemela.
Meli ya MV Uhuru yenye namba za usajili 101242, aina ya Wagon Ferry, mali ya Kenya Railways Corporation (KRC), iliyokuwa inaongozwa na nahodha Leonard Omolo, raia wa Kenya, ikiwa imebeba makaa ya mawe, ilitoka Bandari ya Mwanza Kusini kuelekea Bandari ya Kisumu, nchini Kenya. Katika safari hiyo, meli hiyo iligonga mtumbwi wenye namba za usajili T.2M11 6529 na kuupasua.
Mtumbwi huo ulikuwa na injini aina ya HP 9.9 Yamaha na unamilikiwa na Emmanuel Mjarifu Kakuru.
Wakati wa tukio, ulikuwa umebeba wavuvi wanne ambao ni:Emmanuel Elias ,Malindi William Makeshi ,Peter Masanja na Noel Julias
Kutokana na tukio hilo, mtumbwi ulipinduka na kusababisha wavuvi wote kuzama majini.
Wavuvi wawili waliokolewa, huku wawili ambao ni Noel Julias na Peter Masanja wakizama.
Mnamo tarehe 20 Aprili 2026 majira ya usiku, mwili wa marehemu Peter Masanja ulipatikana.
Jitihada za kumtafuta Noel Julias zinaendelea.
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
April 22, 2026
Rating:

No comments: