test

YESU WA KENYA AZIMIA GAFLA KUKWEPA MSALABA

 Hali ya taharuki imetanda katika kijiji cha Tongaren, Kaunti ya Bungoma, baada ya Eliud Wekesa, maarufu kama “Yesu wa Tongaren,” kukimbizwa hospitalini kufuatia tukio la kuzimia ghafla nyumbani kwake.


Tukio hilo limeto


kea baada ya mamia ya waumini kuvamia makazi yake kuanzia majira ya saa kumi alfajiri jana (10:00 alfajiri), wakishinikiza kiongozi huyo kutimiza kile wanachodai ni "wajibu wake wa kimungu."


Waumini hao, ambao walikusanyika nje ya nyumba yake, walikuwa wamebeba msalaba mkubwa wa mti walioutengeneza wenyewe. Walimtaka Wekesa ajitokeze nje, aubebe msalaba huo, na kuelekea kusulubiwa kwa kuwa anadai yeye ni Mwana wa Mungu.


Inasemekana wafuasi hao wana kinyongo na kiongozi huyo wakimshutumu kwa "kutoroka" zoezi la kusulubiwa wakati wa Ijumaa Kuu ya mwaka uliopita. Safari hii, walisisitiza kuwa hawakuwa tayari kuona tukio hilo likikwama tena.


Hadi sasa, maafisa wa usalama wanajaribu kutuliza ghasia hizo huku hali ya Yesu wa Tongaren ikiendelea kufuatiliwa hospitalini.



YESU WA KENYA AZIMIA GAFLA KUKWEPA MSALABA YESU WA KENYA AZIMIA GAFLA KUKWEPA MSALABA Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on April 04, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.