test

NLD YAITISHA KIKAO CHA KAMATI KUU JUNI 12027

Chama cha National League for Democracy (NLD) kimetangaza kuitisha kikao cha Kamati Kuu kitakachofanyika Julai 1 na 2, 2026 katika Ukumbi wa Popex, Buguruni Sheli, Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam. 



Taarifa hiyo imetolewa kwa wanachama, wadau na umma kwa ujumla ikiwa ni sehemu ya ratiba ya chama ya kujadili masuala muhimu ya kisiasa na kiutendaji.


Kwa mujibu wa taarifa hiyo, ajenda kuu za kikao hicho zitahusisha tathmini ya hali ya chama baada ya uchaguzi, kujadili hali ya kisiasa nchini, pamoja na masuala ya ujenzi na uimarishaji wa chama. 


Aidha, viongozi, wajumbe wa Kamati Kuu na watendaji wa Ofisi Kuu ya chama watapatiwa mafunzo maalumu yatakayolenga kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao.


Kwa mujibu wa taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano ya Umma wa NLD, Pogora Ibrahim Pogora, ambayo imeeleza kuwa kikao hicho ni sehemu ya juhudi za chama kujiimarisha na kuweka mikakati ya utekelezaji wa shughuli zake katika kipindi kijacho.

NLD YAITISHA KIKAO CHA KAMATI KUU JUNI 12027 NLD YAITISHA KIKAO CHA KAMATI KUU JUNI 12027 Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on June 30, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.