test

MHE KHAMBAY AFANYA UZINDUZI WA HUDUMA YA UPASUAJI KITUO CHA AFYA MAISAKA

MHE KHAMBAY AFANYA UZINDUZI WA HUDUMA YA UPASUAJI KITUO CHA AFYA MAISAKA



Mbunge wa Babati mjini Mhe Emmanuel Khambay leo Julai 3,2026 amefanya uzinduzi wa huduma ya upasuaji katika kituo cha afya Maisaka ambacho kina vifaa vya kisasa vya upasuaji



 Khambay alipewa cheti cha pongezi na kituo hicho cha afya kwa kutambua mchango wake toka 2023 ambapo alichangia Viti, meza na mabenchi kwenye kituo hicho


Hata hivyo Mhe Khambay alichangia kiasi cha laki tano kwenye umaliziaji wa jengo la jenereta ambalo linahitaji kiasi cha milioni tano ili kumalizia na kuwahidi kuwaunga mkono kwenye ujenzi wa nyumba ya daktari sambamba na kuanza mchakato wa kutafuta Fedha za umaliziaji wa jengo la kufulia linalohitaji milioni 20, hata kwa kutumia mapato ya ndani ya Halmashauri 



Vilevile Mhe Khambay alitoa mkono wa pongezi kwa wakina mama waliopata watoto kwenye kituo hicho





MHE KHAMBAY AFANYA UZINDUZI WA HUDUMA YA UPASUAJI KITUO CHA AFYA MAISAKA MHE KHAMBAY AFANYA UZINDUZI WA HUDUMA YA UPASUAJI KITUO CHA AFYA MAISAKA Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on July 03, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.