Dareda, Babati DC
13 Julai 2026
Mbunge WA JIMBO la Babati vijijini ambe naibu SPIKA WA BUNGE amefunga rasmi Kambi ya Vijana wa Kizalendo ya Halmashauri ya Wilaya ya Babati iliyofanyika katika Kata ya Dareda,iliyowakutanisha jumla ya vijana 256 kwa muda wa siku tano.
Akizungumza wakati wa hafla ya kufunga kambi hiyo, Mhe. Sillo aliwashukuru viongozi na wananchi wa Kata ya Dareda kwa mapokezi mazuri na ushirikiano waliouonyesha katika kipindi chote cha kambi. Alieleza kufurahishwa na nidhamu uzalendo na hamasa kubwa ya vijana kuelekea shughuli za Mwenge wa Uhuru.
Aidha aliahidi kuendelea kupambania vijana ili wanufaike na fursa mbalimbali zinazotolewa na Serikali, huku akiwahimiza kuwa waadilifu, waaminifu na wachapakazi katika kujenga Taifa.
Akihitimisha hotuba yake, Mhe. Sillo aliwataka vijana kuendelea kuisemea vyema Serikali, kuilinda kwa wivu mkubwa na kuonyesha uzalendo kwa vitendo ili kuendelea kuimarisha maendeleo ya Wilaya ya Babati na Taifa kwa ujumla.
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
July 13, 2026
Rating:


No comments: