test

RC SENDIGA AANZA ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI YA MANDELEO WILAYANI BABATI

 

Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Queen Cuthbert Sendiga, leo Julai 28, 2026, ameanza ziara yake ya ukaguzi wa miradi ya maendeleo katika Wilaya ya Babati kwa kukagua ujenzi wa Zahanati ya Kijiji cha Olasiti.






Zahanati hiyo iliyoanza kujengwa kwa nguvu za wananchi ili kusogeza huduma za afya karibu na wananchi na kupunguza changamoto ya upatikanaji wa huduma hizo. Mradi huo wenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 213 umefikia asilimia 93 ya utekelezaji.











Katika ukaguzi huo, Mhe. Sendiga amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Babati kuhakikisha ndani ya mwezi mmoja, kuanzia Agosti 1, 2026, zahanati hiyo inafikishiwa huduma za umeme na maji ili iweze kuanza kutoa huduma kwa wananchi mara baada ya kukamilika.


















Aidha, Mkuu wa Mkoa amefanya mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Minjingu, ambapo amesikiliza na kutatua kero pamoja na malalamiko mbalimbali yaliyowasilishwa na wananchi.


Ziara ya Mhe. Sendiga inaendelea kwa kukagua miradi ya ujenzi wa zahanati na madarasa katika Kijiji cha Ngoley, kabla ya kuhitimishwa kwa mkutano wa hadhara utakaofanyika Kijiji cha Mwada.









RC SENDIGA AANZA ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI YA MANDELEO WILAYANI BABATI RC SENDIGA AANZA ZIARA YA UKAGUZI WA MIRADI YA MANDELEO WILAYANI BABATI Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on July 28, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.