test

WA NNE WANASWA KWA TUHUMA ZA KUHAMASISHA VURUGU

 Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limewakamata na linaendelea kuwashikilia watuhumiwa wanne kwa tuhuma za kukutwa wakipanga na kuhamasisha watu kufanya vurugu na uhalifu mwingine katika maeneo mbalimbali ya Jijini Mbeya.



Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya Kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi (SACP) Benjamin Kuzaga amewataja wanaoshikiliwa kuwa ni Noah Mwalwange, Mwenyekiti vijana wa CHADEMA vyuoni (CHASO) Mkoa wa Mbeya, Gwamaka Mboka ambaye ni Katibu CHASO Mkoa wa Mbeya, Agustino Wasinyo, Mwenyekiti wa CHASO tawi la CUoM na Rojas Mpwani mwanachuo CUoM.


Watuhumiwa hao walikamatwa Julai 04, 2026 majira ya saa 10 jioni katika eneo la Mafiati lililopo Kata ya Maanga, Jijini Mbeya.


Kamanda Kuzaga amesema ushahidi unakamilishwa ili hatua nyingine za kisheria zifuatwe dhidi ya wanne hao.


Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linatoa wito kwa wananchi kuacha kujiingiza kwenye vitendo vya kupanga na kuhamasisha uhalifu katika mkoani Mbeya kwa maelezo kwamba hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.

WA NNE WANASWA KWA TUHUMA ZA KUHAMASISHA VURUGU WA NNE WANASWA KWA TUHUMA ZA KUHAMASISHA VURUGU Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on July 06, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.