Ligi ya Kijiji Cha mwada kilichopo Kata ya mwada tarafa ya mbugwe wilayani Babati mkoani Manyara imehitimika Leo katika Uwanja wa CCM mwada ambapo TIMU ya mpira ya marinya imeibuka kidedea na kujitwalia kombe Lililo andaliwa.
Ligi hiyo iliyoandaliwa na Halmashauri ya Kijiji Cha mwada imejumuisha VITONGOJI 5 vya Kata ya mwada ambavyo ni Bondeni, mbuyuni Burunge A &B pamoja na makirinya.
Mashindano katika ligi hiyo yamejumuisha mchezo mbalimbali mbali ikiwemo kuvuta kamba, Riadha kufukuza kuku kuvuta kamba n.k,ambapo washindi walipatiwa zawadi mbalimbali.
Katika mpira wa miguu TIMU ya makirinya Fc imeibuka kidedea Kwa goli 3 Kwa mbili DHIDI ya mbuyuni FC na kutwaa kombe la ubingwa.
Akifunga mashindano hayo yaliyoleta hamasa kubwa kwenye jamii na Kwa vijana Kwa Ujumla Kwa niaba ya mbunge wa Jimbo la Babati vijijini na NAIBU Spika wa bunge mhe.Daniel Sillo,Katibu WA Mbunge Bw.Waziri Ramadhani ameipongeza Serikali ya Kijiji Cha mwada Kwa ubunifu huo wa kuanzisha mashindano ya michezo huku akiahidi kufikisha Kwa mbunge Changamoto zilizotajwa,kwenye sekta ya mchezo katika Kijiji hicho.
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
August 30, 2026
Rating:

No comments: