Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. CP Hamduni leo tarehe 15 Septemba, 2026 amempokea na kufanya mazungumzo mafupi na Mhe. Regina Qwaray (MB), Naibu Waziri Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Urumishi wa Umma ja Utawala Bora.
Akizungumza na mgeni huyo Mhe. Hamduni amemweleza Naibu waziri kuwa watumishi mkoani humo wako salama na wanachapa kazi na ofisi yake inawapa ushirikiano wa kutosha ili kuwawezesha kust
awi katika utumishi wao wa umma.
Aidha, amebainisha kuwa Mwanza kwa ujumla wake ipo salama na wananchi wana chakula cha kutosha nyumbani kuwawezesha kuishi kwa amani huku wakiendelea na shughuli za uzalishaji mali hususan katika sekta mbalimbali za kilimo na ufugaji.
Naye, Mhe. Naibu Waziri amebainisha kuwa atakuwepo Mwanza kwa ziara ya kawaida ya kukagua masuala ya kiutumishi na amewasihi viongozi wa mkoa huo kuendelea kuwasikiliza watumishi na kutatua changamoto zao pamoja na kuwapa stahiki zao za kiutumishi wanazostahili kwa mujibu wa sheria.
Vilevile, ameipongeza ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwa kuwapandisha daraja watumishi wanaostahili kwa wakati na kutumia vema mifumo ya utumishi kwani wanarahisisha kufikisha huduma kwa wakati na amesisitiza suala la kuwajengea uwezo watumishi ili waendane na wakati kwenye utendaji kazi.
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
September 15, 2026
Rating:



No comments: