Serikali ya Awamu ya Sita imetoa ajira mpya takribani 45,000 za kada mbalimbali mbalimbali katika bajeti ya mwaka wa fedha 2026/2027
Hayo yameelezwa na Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, *Mhe. Regina Ndege Qwaray, katika ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mhe. Martine Reuben Shigela, katika Halmashauri ya Mji wa Babati.
Mhe. Qwaray amesema pamoja na ajira hizo, Serikali imefanya maboresho makubwa katika Utumishi wa Umma chini ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan*, ikiwemo kuongeza mishahara na kupandisha madaraja na vyeo kwa watumishi.
Aidha, amewaasa wataalam wa Halmashauri ya Mji wa Babati kufanya kazi kwa bidii, akisisitiza kuwa hakuna haki bila wajibu.
JUMLA YA AJIRA 45,000 ZIMETOKEWA NA SERIKALI KATIKA MWAKA WA FEDHA 2026-2027
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
September 25, 2026
Rating:
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
September 25, 2026
Rating:

No comments: