test

SILLO AAHIDI KUPAMBANA NA TATIZO LA MIUNDOMBINU YA BARABARA BABATI VIJIJINI

 



Mbunge wa Jimbo la Babati Vijijini, Mhe. Daniel Sillo, amewahakikishia wananchi wa jimbo hilo kuwa ataendelea kupambana na changamoto ya miundombinu ya barabara.



Mhe. Sillo ameyasema hayo Septemba 26, 2026, wakati akizungumza na wananchi wa Kata ya Dabil.





Amesema jimbo hilo bado lina uhitaji mkubwa wa kuboreshwa kwa miundombinu ya barabara na madaraja.


Ameeleza kuwa barabara ya Gidewari - Mandi imeanza kujengwa, pamoja na barabara ya Seloto - Sabilo


Aidha, katika Kata ya Dabil, Mhe. Sillo ameeleza kuwa kuna mafanikio makubwa katika sekta ya elimu ambapo madarasa yameendelea kujengwa, huku akishukuru Shirika la Karim Foundation kwa kufadhili ujenzi wa madarasa katika kata mbalimbali za Babati Vijijini ikiwemo Dabil.

SILLO AAHIDI KUPAMBANA NA TATIZO LA MIUNDOMBINU YA BARABARA BABATI VIJIJINI SILLO AAHIDI KUPAMBANA NA TATIZO LA MIUNDOMBINU YA BARABARA BABATI VIJIJINI Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on September 27, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.