test

NAIBU WAZIRI REGINA NDEGE AONGOZA MAHAFALI YA 3 YA KIDATO CHA NNE SEKONDARI YA TARAGETY - ATOA MILIONI 2 NA AHADI YA MASHINE YA PHOTOCOPY

 *








Naibu Waziri wa Utumishi na Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Manyara, *Mhe. Regina Ndege*, Oct 8, 2026 amekuwa mgeni rasmi kwenye Mahafali ya 3 ya Kidato cha Nne ya Shule ya Sekondari ya Taragety iliyopo Kata ya Babagara, Halmashauri ya Wilaya ya Babati, Mkoa wa Manyara.


Mhe. Regina aliambatana na Mwenyekiti wa Wazazi Mkoa, *Ndg. Janes Darabe*, Katibu wa UWT Mkoa wa Manyara, *Ndg. Beatrice* na Diwani wa Kata ya Magara, *Mhe. Gonzalez Mkoma*.




Katika kuhamasisha juhudi za masomo, Mhe. Regina alitoa *Shilingi Milioni 2* kama motisha kwa walimu wa shule hiyo


Mhe Regina alitoa ahadi ya kutoa *Photocopy ya Heavy Duty* kwa ajili ya shule, Pia alitoa *mipira na jezi kwa wavulana na taulo za watoto wa kike* kwa wasichana.


Kwa upande wake, Diwani wa Kata ya Magara Mhe. Gonzalez Mkoma, aliongoza harambee ndogo ya kuchangisha fedha za ununuzi wa TV ya shule, ambapo zaidi ya *Shilingi Milioni 1* ilipatikana papo hapo.


*Wito kwa Wazazi Wenye Watoto Wenye Mahitaji Maalum*


Katika hotuba yake, Mhe. Regina alitoa wito mzito kwa wazazi wenye watoto wenye mahitaji maalum kutowaficha majumbani.


Amewataka wazazi kuwapeleka shuleni na kusisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeandaa shule maalum kwa ajili ya watoto hao nchi nzima, huku Mkoa wa Manyara ukiwa na shule hizo, na pia imetoa mafunzo maalum kwa walimu wa watoto wenye mahitaji maalum.

NAIBU WAZIRI REGINA NDEGE AONGOZA MAHAFALI YA 3 YA KIDATO CHA NNE SEKONDARI YA TARAGETY - ATOA MILIONI 2 NA AHADI YA MASHINE YA PHOTOCOPY NAIBU WAZIRI REGINA NDEGE AONGOZA MAHAFALI YA 3 YA KIDATO CHA NNE SEKONDARI YA TARAGETY - ATOA MILIONI 2 NA AHADI YA MASHINE YA PHOTOCOPY Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on October 09, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.