test

DC KAMBANGWA ASISITIZA MADIWANI KUIELEWA MIRADI NA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WAKE IPASAVYO

 

Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Mhe. Mbwana Kambangwa, amewataka Waheshimiwa Madiwani kuhakikisha wanaifahamu vizuri miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao, kuielezea kwa wananchi ili waelewe manufaa yake pamoja na kusimamia kwa karibu utekelezaji wake ili kuhakikisha inakamilika kwa viwango vinavyotakiwa na kuleta tija kwa jamii.



Mhe. Kambangwa ameyasema hayo wakati akizungumza katika kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, akisisitiza umuhimu wa madiwani kuielewa miradi inayotekelezwa katika kata zao ili waweze kutoa taarifa sahihi kwa wananchi na kushiriki kikamilifu katika usimamizi wake.


“Nawaomba sana Waheshimiwa Madiwani, tuhakikishe tunaifahamu vizuri miradi yetu, tuweze kuifafanua kwa wananchi pamoja na kuisimamia vizuri,” amesisitiza Mhe. Kambangwa.





Aidha, amewahimiza madiwani na viongozi wengine kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia sheria, kanuni na misingi ya utawala bora, huku akisisitiza umuhimu wa kuzingatia utu katika kuwahudumia wananchi na kuhakikisha maamuzi yanayofanywa yanazingatia maslahi ya jamii.


Mwisho amesisitiza ushirikishwaji wa wananchi ni nyenzo muhimu katika kuimarisha uwajibikaji, uwazi na usimamizi wa shughuli za maendeleo, hivyo kuwataka viongozi kuhakikisha wanakuwa karibu na wananchi wanaowatumikia.

DC KAMBANGWA ASISITIZA MADIWANI KUIELEWA MIRADI NA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WAKE IPASAVYO DC KAMBANGWA ASISITIZA MADIWANI KUIELEWA MIRADI NA KUSIMAMIA UTEKELEZAJI WAKE IPASAVYO Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on November 13, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.