Mashindano ya Ligi ya Diwani wa Kata ya Magugu, maarufu kama Stan Cup, yamehitimishwa rasmi Novemba 14, 2026, Wilayani Babati.
Mashindano hayo yaliyoandaliwa na Diwani wa Kata ya Magugu, Mhe. Stanley Charles, yalishirikisha timu zaidi ya 15 kutoka katika kata hiyo.
Mashindano hayo yamehitimishwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Hamis Mohammed Mwinjuma, maarufu kama Mwana FA.
Pia alikuwepo Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Regina Ndege Qwaray, ambaye alikuwa mmoja wa wadhamini wa ligi hiyo.
Katika mchezo wa fainali, Manyara Sugar FC waliibuka mabingwa baada ya kuifunga Magugu Rangers mabao 2 kwa 0, na kujitwalia kombe pamoja na zawadi.
Mhe. Hamis Mwinjuma na Mhe. Regina Ndege Qwaray waliwapongeza washiriki wote wa ligi na washindi, kwa kuonyesha nidhamu, vipaji na ushindani wa hali ya juu, huku wakisisitiza umuhimu wa michezo katika kuunganisha jamii na kukuza vipaji vya vijana.
Hongera Manyara Sugar FC kwa kutwaa ubingwa, na hongera Magugu Rangers kwa kufika fainali.
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
November 14, 2026
Rating:






No comments: