test

MBULU WAOMBA FEDHA YA BARABARA KUONGEZA UCHUMI



Halmashauri ya wilaya Mbulu imeomba serikali kuendelea kutoa fedha ili kusaidia kuharakisha ukamilishaji wa ujenzi wa barabara ya Mbulu Hydom hadi Singida pamoja na kipande kinachounganisha  wilaya hiyo  na wilaya ya Hanang kwa kiwango cha Lami ili kuongeza tija katika shughuli za kiuchumi kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kusaidia usafirishaji wa mazao ya kibiashara kwenda kwenye masoko ya nje ya wilaya hiyo.



Akizungumzia umuhimu wa kukamilika kwa barabara hiyo,Mkuu wa wilaya ya Mbulu Mhe. Mbwana Kambangwa katika kikao cha baraza la madiwani cha halmashauri ya wilaya ya Mbulu amesema itasaidia kukua kwa wilaya ya mbulu kiuchumi kutokana na kwamba barabara hii itavutia muingiliano wa wananchi kwa shughuli mbalimbali ikiwemo za kibiashara.


Mkuu huyo wa Wilaya amemtaka Mbunge wa Jimbo la mbulu Vijijini Mhe. Dkt. Emanuel Nuwas kulibeba suala la barabara hiyo kama kipaombele muhimu cha wilaya hiyo na kumkumbusha mara kwa mara waziri wa ujenzi Kadogosa kuhusu kutokuchelewesha fedha za muendelezo wa ujenzi wa barabara hiyo.




"Hata dira ya maendeleo ya taifa ya mwaka 2050 inataja sekta ya usafirishaji kama sehemu nyingine ya kufikia malengo kukuza uchumi" Alisema Kambangwa kwenye kikao hicho.


Katika kuonyesha umuhimu wa ukuzaji wa uchumi wilayani Mbulu  Mbunge wa Jimbo la mbulu Vijijini Emanuel Nuwas ameisisitiza halmashauri kupitia wataalam wake kuanzishwa mkakati wa mazao maalum hususan ya kibiashara yatakayoitambulisha mbulu ndani na nje ya mipaka yake ili kusaidia ukuzaji wa uchumi wa wananchi wilayani hapo.






Kwa Mujibu ya Mbunge huyo na diwani wa viti Maalum katika halmashauri hiyo Narsisi Shishi wamesema kuwa Mbulu inasifika kwa kilimo cha Karoti,Vitunguu swaumu na vitunguu maji pamoja na mazao mengine muhimu hivyo kuongeza umuhimu wa kukamilika kwa barabara hiyo kutoka karate kupitia mbulu hadi thibiti.

 

Aidha halmashauri ya wilaya ya Mbulu imeeleza kuwa licha ya uhitaji wa fedha kwaajilli ya miradi mbalimbali lakini imefanikiwa kuvuka lengo la ukusanyaji wa mapato kwa kufikia zaidi ya 30% katika robo ya kwanza ya mwaka

MBULU WAOMBA FEDHA YA BARABARA KUONGEZA UCHUMI MBULU WAOMBA FEDHA YA BARABARA KUONGEZA UCHUMI Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on November 14, 2026 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.