Jeshi la Polisi Mkoa wa Kilimanjaro kwa kushirikiana na Kikosi Kazi (Task Force) na taasisi ya kuthibiti ubora wa mbegu (TOSCI), limekamata jumla ya kilogramu 737 za mbegu za mahindi zinazodaiwa kukosa ubora, vifungashio, stika pamoja na lebo zinazodaiwa kughushiwa, kufuatia uchunguzi wa malalamiko ya wakulima kuhusu kuuziwa mbegu zisizokidhi viwango katika Halmashauri za Rombo, Moshi na Siha.
Katika operesheni hiyo, mtuhumiwa Mussa Jumanne Idowa, mkazi wa Moshi, anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kutengeneza na kusambaza mbegu zisizo na ubora ndani na nje ya Mkoa wa Kilimanjaro.
Mtuhumiwa huyo alikamatwa Novemba 2, 2026, kwa tuhuma za kununua mahindi ya kawaida, kuyapaka rangi na kuyafungasha katika vifungashio vya kampuni mbalimbali za mbegu, zikiwemo SEEDCO, BAYER LIFE SCIENCE na CORTEVA AGRI-SCIENCE, kisha kuyasambaza kwa wakulıma.
Aıdha, anadaıwa kuingıza mbegu kutoka nchı jıranı bıla kutuata taratibu za taasisi ya Uthibiti na Usimamizi wa Ubora wa Mbegu (TOSCI).
Katika hatua hiyo, vilikamatwa vifungashio 7,770 vikiwemo 5,939 vya SEEDCO na 1,831 vya BAYER LIFE SCIENCE, vifungashio 241 vilivyokwisha kutumika vya kampuni ya BAYER LIFE SCIENCE, stika 260 zinazodaiwa kuwa bandia za kampuni ya BAYER LIFE SCIENCE aina ya DKC.80-33, pamoja na lebo 3,000 zinazodaiwa kughushiwa za TOSCI.
Vifungashio na lebo hizo zinadaiwa kutumika kuwahadaa wakulima kuhusu ubora na uthibitisho wa mbegu hizo.
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
November 16, 2026
Rating:

No comments: