Jeshi la Polisi Kanda Maalum
ya Dar es salaam limeonya dhidi ya Makundi ya Watu wanaodaiwa kuhamasishana kufanya vurugu, fujo na vitendo vya kihalifu ifikapo Novemba 6, 2026 siku ya hukumu ya Mwenyekiti wa CHADEMA, Tundu Lissu.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, SACP Jummane Muliro amesema wamepokea taarifa za kuwepo kwa baadhi ya Watu ndani na nje ya Dar es salaam wanaohamasishana kusafiri kwenda Jijini humo siku hiyo, huku baadhi yao wakidaiwa kuwa na nia ya kufanya fujo na vurugu.
Jeshi hilo limeeleza kuwa linatambua haki ya Wananchi kufika Mahakamani, likisisitiza kuwa maeneo ya Mahakama yanajulikana na yana uwezo wa kuhudumia Watu wanaohitaji kufika kwa ajili ya shughuli za kisheria.
Hata hivyo, Polisi limeonya kuwa halitavumilia Makundi au Watu watakaobainika kupanga au kuhamasisha vurugu, hujuma na vitendo vingine vya kihalifu kwa kutumia siku hiyo kama fursa.
MULIRO: TUMEJIPANGA SIKU YA HUKUMU YA LISSU
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
November 03, 2026
Rating:
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
November 03, 2026
Rating:

No comments: