test

BENKI YA MWANGA HAKIKA WAZINDUA TAWI JIPYA ARUSHA

 


Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba (wa pili kulia) na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Mwanga Hakika  Bank Eng. Ridhiwan Mringo  (wa pili kushoto) wakifungua Kitambaa cha jiwe la Msingi kuashiria Ufunguzi wa tawi jipya na la kisasa jijini Arusha,Wanaoshuhudia pembeni ni kutoka kulia ni  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya MHB, Jagjit Singh ,Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Felician Mtehengerwa na  Mstahiki meya Arusha Maximilian Iranghe , Hafla ya uzinduzi ilifanyika mwishoni wa wiki iliyopita .

Baadhi ya wageni waalikwa na wafanyakazi wa Benki ya Mwanga Hakika wakifuatilia hotuba ya mgeni rasmi Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba , Hafla ya uzinduzi ilifanyika mwishoni wa wiki iliyopita .
Waziri wa Fedha na Mipango Dk. Mwigulu Nchemba (wa pili kulia) akikata utepe kuashiria Ufunguzi wa tawi jipya na la kisasa jijini Arusha,Wanaoshuhudia pembeni ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Mwanga Hakika  Bank Eng. Ridhiwan Mringo,  Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya MHB, Jagjit Singh ,Mkuu wa Wilaya ya Arusha, Felician Mtehengerwa na  Mstahiki meya Arusha Maximilian Iranghe , Hafla ya uzinduzi ilifanyika mwishoni wa wiki iliyopita .

 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Mwanga Hakika  Bank Eng. Ridhiwan Mringo akitoa hotuba katika hafla ya ufunguzi wa tawi jipya Jijini Arusha

 

Arusha. Aprili 28,  2023: Benki ya Mwanga Hakika (MHB) leo imezindua tawi jipya na la kisasa jijini Arusha, ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kutanua mtandao wake wa huduma za kifedha nchi nzima.

Tawi hilo jipya lililopo katika jenga la Central Plaza, barabara ya Sokoine jirani na Clock tower jijini Arusha, linafanya idadi ya matawi ya benki hiyo kufikia saba. Matawi mengine yapo Dar es Salaam, Moshi, Dodoma, Mwanga na Same.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa tawi hilo, mkurugenzi mtendaji wa benki hiyo  Jagjit Singh alisema tawi hilo litaweza kurahisisha huduma kwa wateja wake na wakazi wa Arusha kwa ujumla.

“Tawi hili la hapa Arusha litarahisisha upatikanaji wa huduma za kifedha kwa kuwa lipo kati kati ya jiji. Tawi ni la kisasa na lina sehemu maalum kwa ajili ya wateja wakubwa, vifaa vya kisasa, huduma ya kubadilisha fedha nakadhalika. Hii yote ni kuhakikisha kuwa  wateja wetu wanapata huduma bora za kisasa na kwa urahisi,” alisema

Mkurugenzi huyo aliongeza kuwa tawi hilo limefunguliwa mahsusi kwa ajili ya kuhakikisha kuwa fursa za kiuchumi zilizopo jijini Arusha zinaweza kuwafaidisha wakazi wa jiji hilo.

 “Tawi linalozinduliwa leo ni sehemu ya mkakati wetu wa kujitanua na kuwafikia wateja wengi zaidi. Lengo letu ni kuwafikia wateja popote pale walipo lakini pia tukizingatia utoaji wa huduma bora za kifedha zinazoendana na mahitaji yao,” alifafanua.

 

Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu Nchemba aliipongeza benki hiyo kwa kujikita katika kutoa huduma kwenye miradi ya miundo mbinu na kufanya kazi na  wajasiriamali wadogo na wakati

“Napenda kuipongeza benki ya Mwanga Hakika kwa jitihada zake za kujitanua na hivyo kutoa fursa za wananchi wa kada mbali mbali kufikiwa na huduma za kifedha pamoja na kusaidia swekta mbali mbali ikiwamo ujenzi wa miundo mbinu,” alsema

ENDS

BENKI YA MWANGA HAKIKA WAZINDUA TAWI JIPYA ARUSHA BENKI YA MWANGA HAKIKA WAZINDUA TAWI JIPYA ARUSHA Reviewed by Adery Masta on April 29, 2023 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.