test

MATI SUPER BRAND YAZIDI KUSHIKA KASI MANYARA

  Na Fadhili Shabani, Babati Manyara.


Kulia ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Mati super brand's Bw. David Mulokozi akipokea Moja ya kikombe kutoka kwa Mkuu wa mkoa wa Manyara Mh. Makonongoro Nyerere kushoto ni Doreen Mushi Afisa rasilimali watu Katika kampuni hiyo akiwa ameshika kati ya vikombe vilivyo twaliwa na kampuni ya Mati Super brand's.




Matukio Katika picha maandamano ya Mati Super brand's Siku Ya Mei Mosi Manyara

.....................................................................................................................

Kampuni ya Mati super brand's inayo jihusisha na vinywaji changamshi, ikiwemo sed pineapple flovour gin, Strong dry gin, strong coffee, Tanzanite vodka na Tai Original imeendelea kung'aa maraa Baada vikombe mbalimbali Katika Maadhimisho ya siku ya wafanyakazi duniani mei mosi Kwa mkoa wa Manyara.

Akizungumza na waandishi wa habari mara Baada ya kushinda vikombe hivyo meneja mauzo na masoko wa kampuni ya Mati super brand Gwandumi Mpoma amesema Siri ya ushindi huo ni kutokana na ushirikiano uliopo baina ya wafanyakazi na uongozi wa kampuni hiyo.

Hata hivyo Mpoma amesema kampuni ya Mati super brand imekuwa ikiwajali wafanyakazi wake Kwa kuwajengea mazingira Rafiki ndani na nje ya kazi ikiwa ni pamoja na kuwalipa mishahara Kwa wakati.

Sanjari na hayo meneja mauzo na masoko wa kampuni hiyo ametoa wito Kwa makampuni mengine mengine kuiga mfano wa mati kwa kuwajali wafanyakazi wao.

Ikumbukwe kwamba vikombe ambavyo kampuni ya mati imeshinda Katika madhisho hayo ni pamoja na kuongoza Katika maandamano, mabanda ya maonyesho ya bidhaa pamoja na wafanyakazi kazi Bora.



MATI SUPER BRAND YAZIDI KUSHIKA KASI MANYARA MATI SUPER BRAND YAZIDI KUSHIKA KASI MANYARA Reviewed by Adery Masta on May 05, 2023 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.