test

TIGO WAANZA KUMWAGA MAMILIONI KWA WASHINDI WA "CHA WOTE " , TAZAMA HAPA NAMNA YA KUSHINDA ( + VIDEO )

 Na Mwandishi Wetu.

 Ikiwa ni Takribani wiki sasa tangu kampuni ya Mawasiliano ya Tigo izindue Kampeni yake ya CHA WOTE yenye lengo la kuwasaidia wateja wa Tigo kutimiza malengo yao waliojiwekea ndani ya mwaka huu , ambapo wateja 320 kila siku wanajishindia zawadi mbalimbali ikiwemo Fedha Taslimu hadi Milioni Moja kwa kufanya miamala tu kupitia TigoPesa.

Akizungumza wakati wa Kuwakabidhi Mfano wa Hundi Baadhi ya Washindi wa Milioni Moja Moja , Meneja wa Wateja Maalum Tigo Pesa Bi. Mary Rutta amesema kuwa hadi sasa ikiwa ni wiki moja tu tangu Kampeni iyo izinduliwe wameshapatikana washindi Takribani 2240 kutoka maeneo mbalimbali nchini .

" Leo tunayo furaha kubwa kuwa na baadhi ya washindi wa Kampeni yetu ya CHA WOTE ambao hawa ni washindi wa Milioni Moja , Lakini niwakumbushe Watanzania kwamba kila siku tunatoa zawadi ikiwemo pesa taslimu hadi Milioni Moja kwa washindi 320 ,kuibuka mshindi ni rahisi tu unachotakiwa ni kufanya miamala na Tigo Pesa kama Kutumia Lipa Kwa Simu , Kununua Vifurushi , Kulipia Bili kwa Tigo Pesa , n.k kwa kufanya ivyo nawewe siku si nyingi utakua miongoni mwa Washindi wa Kampeni hii ya CHA WOTE ". Alisema Bi. Mary Rutta.

Baadhi ya Washindi waliokabidhiwa Hundi ya Milioni Moja kila mmoja leo hii ni Rajabu Shabani Mkazi wa Mkata Morogoro , Nella Mushi Mfanyabiashara wa Vipodozi Tabata Dar Es Salaam , Revina Byabato Mkazi wa Sinza Dar Es Salaam , na Mgolozi Baitan ambao nao wameelezea Furaha waliyonayo kuwa miongoni mwa washindi wa Kampeni hii ya CHA WOTE.


TIGO WAANZA KUMWAGA MAMILIONI KWA WASHINDI WA "CHA WOTE " , TAZAMA HAPA NAMNA YA KUSHINDA ( + VIDEO ) TIGO WAANZA KUMWAGA MAMILIONI KWA WASHINDI WA "CHA WOTE " , TAZAMA HAPA NAMNA YA KUSHINDA ( + VIDEO ) Reviewed by Adery Masta on June 30, 2023 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.