test

ONE MAP AFRICA KUVUTIA UWEKEZAJI NCHINI ( + VIDEO )

 



Mwanzilishi wa Kampuni ya ONE MAP AFRICA Bwn. Joseph John Ng'wandu ( katikati ) katika picha ya pamoja na Mchekeshaji Maarufu Nchini JK COMEDIAN na Mwakilishi wa Mwanzilishi mwenza wa Kampuni hiyo Bi. Jamila Ngonyani , Muda mfupi baada ya uzinduzi wa Kampuni iyo ambayo inajihusisha na masuala ya Diplomasia ya Uchumi kwa lengo la kutangaza fursa za uwekezaji zinazopatikana nchini kimataifa kupitia tafiti na kutafuta masoko ya bidhaa za Tanzania kwenye soko la kimataifa. 

***************************************************

Wahitimu wa Chuo cha Diplomasia Kurasini Bwn. Joseph John Ng'wandu na Bwn. Augustino Yohana Ngull wamezindua Kampuni yao iitwayo ONE MAP AFRICA ADVISORY PANEL LIMITED Kampuni itakayojikita zaidi na Utafiti wa Masoko ya nje ya Bidhaa za Tanzania ikiwemo pia  kuwasaidia vijana na wawekezaji kutoka ndani na nje ya nchi , kung'amua fursa mbalimbali za uwekezaji ndani ya nchi ya Tanzania ikiwemo kuwasaidia katika michakato ya Usajili wa Biashara na makampuni yao.

Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar Es Salaam muda mfupi baada ya kuzindua kampuni hiyo  Bwn. Joseph John Ng'wandu ameomba ushirikiano kwa serikali pamoja na Taasisi zake ikiwemo wizara ya Kilimo , Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano na Kimataifa , na Wizara ya Uwekezaji Viwanda na Biashara ili waweze kufikia lengo lao kwa Maendeleo ya Taifa la Tanzania.


ONE MAP AFRICA KUVUTIA UWEKEZAJI NCHINI ( + VIDEO ) ONE MAP AFRICA KUVUTIA UWEKEZAJI NCHINI ( + VIDEO ) Reviewed by Adery Masta on July 01, 2023 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.