RC SENDIGA atoa Wito kwa wakurugenzi,mainjinia,maafisa elimu taaluma pamoja na wakaguzi wa elimu kuwa na matumizi sahihi ya pesa katika kuboresha sekta ya elimu.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake mkuu wa mkoa wa MANYARA Mhe. QUEEN SENDIGA amesema mpaka sasa amepokea sh bilioni 6.417 kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu mkoa wa Manyara hivyo ni vyema wakurugenzi.mainjinia.maafisa elimu taaluma pamoja na wakaguzi wa elimu kuwa na usimamizi mzuri wa pesa hizo ili ziweze kuwa na manufaa katika jamii.Aidha SENDIGA amesema pia mkoa wa manyara upepata ongezeko la walimu 246,walimu wa shule ya msingi 168 na waalimu wa sekondary 78 na mpaka sasa walimu 240 wamesharipoti na wachache waliobaki wataripoti muda si mrefu.
Mkuu wa Mkoa wa MANYARA QUEEN SENDIGA amewataka wakurugenzi,mainjinia,maafisa elimu taaluma pamoja na wakaguzi wa elimu kusimamia vyema pesa zilizotolewa kwa ajili ya kuboresha sekta ya elimu.
RC SENDIGA AWAPA MTIHANI WAKURUGENZI , MAINJINIA , MAAFISA ELIMU NA WAKAGUZI WA ELIMU
Reviewed by VISIONMEDIA
on
July 03, 2023
Rating:
No comments: