Mkuu wa Wilaya ya Hanang' Bi Janeth Mayanja amefika Kata ya Balangdalalu akiwa na Wataalamu kutoka Bonde la Kati Singida, TFS, na Halmashauri kusikiliza kero na kutatua mgogoro wa baadhi ya Wananchi walioanzisha shughuli za kilimo Ziwa Balangdalalu ndani ya mita 60 na eneo lenye maji chini ya ardhi yaani (underground water)
Wananchi wa Vijiji vyote vinavyozunguka Ziwa wameombwa kutunza mazingira ya asili ya eneo hilo kwa manufaa ya vizazi vinavyokuja kwani lina maji yanayoonekana kwa macho na maji yaliyopo chini ya ardhi na kuacha kukata miti iliyodumu kwa miaka mingi kwani ni kichocheo cha upekee kwa Ziwa Balangdalalu.
Aidha Mayanja amewashukuru Wataalamu wa Bonde kwa kazi kubwa wanayoifanya ikiwemo kuweka beacon katika maeneo hayo na amewaomba Wananchi kuunga mkono jitihada za Serikali za kutunza eneo hilo.Aidha Mkuu wa Wilaya baada ya kumaliza mgogoro wa uharibu wa mazingira ya Ziwa Balangdalalu alisikiliza kero mbalimbali.
No comments: