Jeshi la Polisi Mkoa wa Manyara limekuja na mbinu ya kufanya doria na patro za gari njia kuu usiku na mchana ili kuzuia ajali na kuwakamata madereva wanaovunja Sheria za usalama barabarani hasa nyakati za usiku
Hayo amesema Kamanda wa Polisi Mkoa ni humo Kamishna Msaidizi wa Polisi George Katabazi wakati akipokea gari aina ya Pro Box PT 1486 kwa ajali ya kuimarisha doria njia kuu
Gari Hilo lenye dhamani ya zaidi ya Milioni 19 limetolewa na Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Manyara
Akikabidhi gari Hilo Kaimu mwenyekiti wa Kamati John Methew amesema gari hili litasaidia kufanya doria barabarani na kuzuia ajali hasa katika maeneo korofi kama kona za Kolo na milima ya Logia
Naye Mkuu wa Kikosi Cha Usalama Barabarani Mrakibu wa Polisi Fredric Mpolo amewataka askari wa kikosi hicho kuongeza Kasi ya kutoa elimu kwa madereva na watumiaji wengine wa barabara ili kuzuia ajali
Mpolo awaihakikishia kamati hiyo kuwa gari litatumika kufanya doria njia kuu na
Reviewed by VISIONMEDIA
on
September 13, 2023
Rating:
.jpg)
No comments: