test

DC-MBULU AKUTANA NA ASKOFU WA KKKT DAYOSISI YA MBULU.*


                                           


  


Mkuu wa wilaya ya Mbulu Komred Kheri James, Mapema leo amefanya ziara katika  makao makuu ya KKKT Dayosisi ya Mbulu na kufanya mazungumzo na Baba Askofu Nicholous Nsanganzelu wa Dayosisi hiyo.                                                           


Katika mazungumzo hayo Komred Kheri James ameupongeza uongozi wa KKKT - Mbulu kwa ushirikiano mkubwa uliopo baina yao na Serikali katika sekta ya Afya, Elimu naa Ustawi wa Jamii.                                                  


Aidha Komred Kheri James ametumia fursa hiyo kuliomba kanisa kuunganisha nguvu katika kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia, Mmomonyoko wa maadili, malezi bora ya jamii, uhamasishaji wa shughuli za maendeleo na kushiriki kikamilifu katika ajenda ya kuijenga wilaya ya Mbulu kichumi na kijamii kwa faida ya Wananchi.                                           


Pamoja na mambo mengine Komred Kheri James amepata fursa ya kutembelea ujenzi wa mradi mkubwa wa jengo la kitega uchumi cha kanisa linalo tarajiwa kuwekewa jiwe la msingi hivi karibuni na Mkuu wa Kanisa KKKT Dkt. Alex Malasusa.      


Komred Kheri james amewapongeza viongozi na waumini wa Dayosisi ya Mbulu kwa ubunifu wa mradi mkubwa wa kitega uchumi utakao kuwa kichocheo cha huduma na biashara katika wilaya.                             


Aidha Komred Kheri James amemhakikishia Baba Askofu Nicholous Nsanganzelu ushirikiano wa kutosha katika kuendelea kuwahudumia na kuwatumikia wananchi wa Mbulu katika sekta zote za muhimu kwa jamii.                     


 *#Kwapamoja,Tunaijenga Mbulu yetu.*

DC-MBULU AKUTANA NA ASKOFU WA KKKT DAYOSISI YA MBULU.*  DC-MBULU AKUTANA NA ASKOFU WA KKKT DAYOSISI YA MBULU.*    Reviewed by VISIONMEDIA on September 12, 2023 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.