J
eshi la Polisi Mkoa wa Manyara limewata wananchi wenye Nia ya kutenda vitendo vya uhalifu kuacha mara Moja kwani wamejipanga kuzuia na kupambana na wahalifu WA aina yoyote Mkoani humo
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara Kamishna Msaidizi wa Polisi George Katabazi wakati akizungimza na waandishi wa habari 27 Septemba 2023 mara baada ya mazoezi ya utayari
Katabazi ameongezea kuwa mazoezi haya ni ya kawaida na lengo lake ni kuwaonesha wananchi kuwa Jeshi Hilo Lilo imara madhubiti wakati wowote kukabiliana na matishio ya kiuhalifu wa wahalifu
"Lengo la kupita katika mitaa tukiwa na silaha za moto sio kuwatisha wananchi ni kuonesha nguvu tulionayo ya kukabiliana na wahalifu na kuzuia uhalifu" amesema Katabazi
Jumla ya Maafisa wakaguzi na askari wa vyeo mbalimbali 120 wamepita katika mitaa ya mji wa Babati wakiwa na Magari na silaha mbalimbali kwa lengo la kuionesha jamii kuwa ulinzi wao na Mali upo salama
JESHI LA POLISI MANYARA LATOA ONYO KALI KWA WAHALIFU
Reviewed by VISIONMEDIA
on
September 28, 2023
Rating:
No comments: