test

TBA kuin'garisha GEITA, kujenga jengo la Biashara na makazi


 



Na Mary Margwe Geita 


Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Constantine Kanyasu amewapongeza Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Kwa kua na matarajio ya kujenga jengo Moja la gorofa litakalohusisha Biashara na makazi Mjini Geita.


Pongezi hizo zimekuja Kufuatia mbunge huyo kutaka kujua endapo  nje ya miradi ya ujenzi wa majengo ya ofisi za umma wakala huyo kama ana mpango wa kuwekeza miradi ya nyumba za makazi mjini Geita kama ilivyo katika mikoa mingine kama Dodoma.


Mbunge Kanyasu alitoa pongezi hizo Jana alipotembelea katika banda hilo katika maonesho ya sita ya teknolojia ya madini yanayaofanyika  katika viwanja vya EPZA Bombambili Halmashauri ya Mji Geita.


Akijibu swali hilo Kaimu Meneja Mawasiliano na Masoko - TBA, Fredrick Kalinga amesema katika Mwaka wa fedha 2023/2024  TBA ina mpango wa kuanza ujenzi wa jengo Moja la ghorofa katika eneo la raund about Msikitini, ambapo chini litakuwa Kwa Matumizi ya Biashara na juu litakua kwaajili ya makazi.



"Mheshimiwa Mbunge katika bajeti ya mwaka huu tunatarajia kujenga jengo Moja la ghorofa pale eneo la round about maarufu msikitini na taratibu zote zimekamilika na muda wowote tutaanza ujenzi wake "amesema Kalinga.


Aidha Kalinga ameongeza kuwa Serikali ya awamu ya sita imeona haja ya kuhuisha Sheria iliyoanzisha TBA kwa kuiboresha kupitia GN namba 595 ya tarehe 25 Agosti 2023 ambayo inairuhusu TBA kushirikiana na Sekta Binafsi kuendeleza miliki nchini kwa kujenga nyumba za kupangisha na kuuza kwa wananchi wote, hivyo kwa kushirikiana na Sekta Binafsi, TBA inatarajia kujenga nyumba nyingi za kuuza na kupangisha kwa wananchi wote.


Kwa kufanya hivyo itakua nafasi nzuri ya kuendeleza majengo mengi zaidi na tunatarajia taasisi itaongeza uwezo wake wa kutekeleza miradi mingi zaidi ya ujenzi wa nyumba za makazi, ambapo muda si mrefu Sekta Binafsi itaarifiwa namna gani watashirikiana na sisi TBA"ameongeza Kalinga


Kalinga ameongeza kuwa kuna miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na mingine tayari imeshakamilika kama hospital ya rufaa ya Kanda Chato, hospital ya rufaa ya mkoa na majengo ya Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Geita na wakuu wa Wilaya wa Mbogwe na Nyang’wale.


Kwa upande wake mbunge huyo wa Geita mjini amewapongeza TBA kwa kazi nzuri wanazozifanya na kuwakaribisha katika uwekezaji mbalimbali mjini humo.

TBA kuin'garisha GEITA, kujenga jengo la Biashara na makazi TBA  kuin'garisha GEITA, kujenga jengo la Biashara na makazi Reviewed by VISIONMEDIA on September 28, 2023 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.