test

Mbunge Kanyasu atembelea banda la Brela na kupongeza jitihada zinazofanywa na Wakala wa Usajili wa Biashara na leseni ( BRELA )

 Na Mary Margwe, Geita





MBUNGE wa Jimbo la Geita Mh. Constantine Kanyasu amewapongeza Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA) kwa kuendelea kutoa Elimu kwa wadau kikamilifu Kwa wananchi mbalimbali ambao wamekuwa wakitembelea kwenye banda lao kwa lengo la kujua majukumu ya taasisi hiyo.


Kanyasi amebainisha hayo leo Septemba 26, 2023 Mkoani Geita mara baada ya kutembelea kwenye banda la Brela lililopo kwenye Maonesho ya Sita ya  ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini chini ya kauli mbiu " Matumizi ya Teknolojia sahihi katika kuinua wachimbaji wadogo kiuchumi na kuhifadhi Mazingira"  yanayofanyika katika viwanja vya EPZA Bombambili Halmashauri ya Mji Geita


Naye Mkuu wa Sehemu ya Majina ya Biashara (Brela) Bw. Harvey Godwin Kombe akimueleza majukumu ya Brela Mbunge wa Jimbo la Geita Mheshimiwa Constantine Kanyasu mara baada ya kutembelea banda lao katika Maonesho ya Sita ya Madini yanayoendelea kwenye viwanja vya EPZA Halmashauri ya Mji wa Geita Leo Septemba 26, 2023.

Mbunge Kanyasu atembelea banda la Brela na kupongeza jitihada zinazofanywa na Wakala wa Usajili wa Biashara na leseni ( BRELA ) Mbunge Kanyasu atembelea banda la Brela na kupongeza jitihada zinazofanywa na Wakala wa Usajili wa Biashara na leseni ( BRELA ) Reviewed by VISIONMEDIA on September 28, 2023 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.