Na Mary Margwe, Geita
Mkurugenzi wa Uchumguzi wa bidhaa na Mazingira kutoka Mamlaka ya Maabara na Mkemia Mkuu wa Serikali Sabanitho Mtega amewataka Wachimbaji wadogo kuhakikisha wanatumia vifaa kwa ajili ya kujikinga ili kuepukana na madhara yatokanayo na kemikali wanazotumia wakati wa utafutaji wa madini.
Hayo alibainisha jana wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye maonyesho ya sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini chini ya kauli mbiu " Matumizi ya Teknolojia sahihi katika kuinua wachimbaji wadogo kiuchumi na kuhifadhi Mazingira" yanayofanyika katika viwanja vya EPZA Bombambili Halmashauri ya Mji Geita.
Mtega alisema tatizo kubwa linalowakabili wachimbaji wadogo wa Madini ni kutumia kemikali bila kuvaa vifaa vya kuzuia ama kujilinda afya zao,hali inayowapelekea baadaye kupata madhara ya kiafya.
" Kwenye tasnia ya Madini, kwenye utafutaji wanatumia kemikali, kwenye uchimbaji pia wanatumia kemikali, hivyo wachimbaji wadogo wanatakiwa kuhakikisha wanalinda afya zao kuliko kitu chochote kile, ili kuweza kuendelea nanshughuli za uchimbaji ulio salama" amesema Mtega.
Kitendo Cha kutumia kemikali bila kuvaa vifaa vya kujikinga na wazi mchimbaji anakua amejikatiantamaa na maisha yake, huku bila kujua kuwa afya njema ndio mtaji katika maisha, hivyo ni vema wakahakikisha wanazingatia hilo ili kujihakikishia Usalama wao kkazini.
" Sisi tunaendelea kuwasisitiza wachimbaji wadogo wadogo wanapofanya shughuli zao za uchimbaji kwanza watambue kemikali wanazotumia lakini pia wajue madhara yake na mwisho wachukue hatua kwa maana ya kutumia vifaa vya kujikinga ili waweze kubaki salama" amefafanua Mtega.
Kufuatia hilo amewataka idha wachimbaji wadogo na wananchi kiujumla kuweza kutembelea banda lao na kupata elimu stahiki itakayowawezesha kuepukana na madhara mbalimbali yatokanayo na matumizi ya kemikali kwani kuna umuhimu mkubwa wa kupatamtaarifa za kimaabara.
Akizungumzia lengo la uwepo wao katika Maonyesho ya sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini, amesema Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ndio Mamlaka ya udhibiti katika masuala ya Usimamizi na matumizi ya kemikali za viwandani na majumbani, hivyo wananumuhimumwa mkubwa wankuweponnankutoanelimumkwanjamii.
" Kama tunavyofahamu tasnia ya uchimbaji na utafutaji wa Madini unahusisha sana matumizi ya kemikali na sisi tukiwa kama Mamlaka ya udhibiti tunapaswa sasa kutoa elimu kwa umma ili kemikali zinapotumika zitumike kwa utaratibu ulio salama bila kuleta madhara kwa afya na Mazingira" amefafanua Mtega.
Akielezea majukumu Mtega amesema, Mamlaka ya Maabara Mkemia Mkuu wa Serikali ni Taasisi iliyo chini ya Wizara ya afya yenye jukumu la kufanya uchunguzi wa sampuli mbalimbali na kutoa ushauri kwa Mamlaka za Mdhibiti.
"Baadhi ya sampuli ambazo tunafanya ni kubaini ubora na Usalama wake kama vile vyakula, kemikali , sampuli zinazohusiana na Usalama kazini, lakini pia sampuli zinazohusiana na Uchaguzi wa Mazingira" amesema Mtega.
Aidha amesema pamoja na majukumu hayo lakini pia wanasimamia sheria ya kudhibiti Teknolojia ya vina saba vya binadamu, chini ya sheria hiyo mkemia Mkuu wa Serikali ndiye mwenye Mamlaka ya kudhibiti Teknolojia hiyo nchini.
" Mtu akitaka kufanya utafiti juu ya vina saba vya binadamu, basi Mamlaka inatoa vibali kwa ajili ya kuwawezesha watafiti kuendelee na tafiti zao katika maeneo haya" amesema Mtega.
Akielezea miongoni mwa changamoto wanazokutana wakati wakitoa huduma kwa wananchiamesema nimpamoja na uelewa duni wa sheria na majukumu ya Mamlama ya Maabara Mkemia Mkuu wa Serikali.
"Sheria ya Usimamizi wa udhibiti kemikali ya na. 182 inawataka wadau wote wanaojihusisha na Biashara ya kemikali wasajiliwe lakini kama wote hawajui utaratibu za kusajili kwake inakua ni changamoto, hivyo wafike ili waonfokane na changamoto na hatimaye kuwa fursa.
No comments: