Tume ya Madini ije na Teknolojia ya kukamata Madini ya dhahabu, Shaba na mengine-Mbunge Kanyasu

test

 Na Mary Margwe, Geita

Mbunge wa Jimbo la Geita Mjini Mh. Constantine John Kanyasu ameiomba Tume ya Madini kuwasaidia kuja na Teknolojia mpya ya kuanza kukamata Madini ya Dhahabu, ( Gold), Shaba ( Silva)   na Madini mengine ili wasitupe utajiri huo kwenye matope.

Kanyasu ameyasema hayo Jana kwenye Maonyesho ya sita ya Kimataifa ya Teknolojia ya Madini chini ya kauli mbiu " Matumizi ya Teknolojia sahihi katika kuinua wachimbaji wadogo kiuchumi na kuhifadhi Mazingira"  yanayofanyika katika viwanja vya EPZA Bombambili Halmashauri ya Mji Geita.

Amesema Madini mengi yamekua yakiishia kwenye matope kwa kukosa Teknolojia ya kuanza kukamata Madini ya dhahabu, Shaba pamoja na Madini mengine 

" Sasa hapa tuna Madini yanayotupwa, kule wanaofanya uchechuaji wanakamata zaidi dhahabu na Silva, maana Silva nyingí inabaki kwenye tope, waje na Teknolojia ya kukamata silva inayobaki kwenye tope, kwasababu sokoni tunahitaji Silva lakini sio koo kwa mchimbaji, mchimbaji anatafutwa dhahabu kwa hiyo asilimia anayopatikana baada ya kuchenjuliwa ni ile ambayo imekamatwa kwa bahati mbaya" amesema Kanyasu.

Aidha Kufuatia hilo ameiomba Tume ya Madini kuwasaidia kuja na usaidia kuja na  Teknolojia mpya ya kuanzia kukamata  Madini ili wasitupe utajiri huo kwenye matope na Madini mengine kama hapa walivyokuja hapa watu wa Tanzanite kutoka Mirerani tumefurahi sana, kwasaba na Geita yapo mawe aina hii ambayo yanaweza kufanyika nakshi watu wakanunua wakavaa, wakaacha kuvaa  maplastiki" amesema Kanyasi.

Aidha amesema kadiri Geita inavyoonekana ilivyo sasa sivyo ilivyokua zamani, kuanzia Kasama mpaka Geita amjini palikua na msitu Mkubwa sana, lakini  miti yote imekwisha kwasababu ya Uchimbaji wa madini ( Matumizi ya Matimba) 

" Sasa iko haja ya kutafuta Teknolojia itakayookoa Misitu itakayobaki ili tusiendelee kukata miti yote inayobaki tutaharibu hali ya hewa, kuna Uhusiano mkubwa wa hali ya hewa ya Kanda ya ziwa na Misitu ya asili iliyokuwepo, kwahiyo tuchimbe Madini tutengeneze pesa, zile pesa zirudi kupanda miti" amesema Mbunge Kanyasu.

" Kazi nzuri imefanywa na Wizara ya Maliasili na Utalii pale mbele ya Katolo ule msitu wa Bihalamulo wamepanda hekta 69,000 pale wamepanda msitu mkubwa, ifanyike hivyo kwenye maeneo yote yaliyokua na msitu wa asili lakini imevunwa kwenda kwenye madini kwaajili ya kufidia ile Misitu ambayo imeharibika, Mimi nafikiri kwakufanya hivyo tutaendelea kuwa salama zaidi Kwa hali hiyo" ameongeza.

Aidha amesema jambo pekee ambalo wananchi wanatakiwa kujua ni kwamba bado walengwa ( wachimbaji wenyewe ) ado hawajafikiwa  kiasi cha kutosha.

" Ziko Kampuni ambazo lazima wawafuate wachimbaji madogo kule chini, Maonyesho haya hawawalengi makampuni makubwa kama GGM, Bakrifu, na Sota Mining, yanalenga wachimbaji wadogo kwahiyo tuangalie namna ya kuwafuata wale wachimbaji wadogo kule chini hasa  kwenye kuwapeleka Teknolojia, mitaji, lakini kwenye kuwawekea bima " amefafanua Mbunge Kanyasu.

" Kwasababu mabosi wamekuja hapa,  lakini wale wachimbaji wenyewe wako kwenye mashimo, ambao hata hawajapata nafasi ya kuja  kuona Maonyesho haya licha ya kuwa wao ndio wahusika wakuu, na ndio wanaokufa kwa kuangukiwa na miamba" amesema Mbunge Kanyasu

Aidha Mbunge huyo ametumia fursa hiyo kuwapongeza waandaaji wa Maonyesho hayo na pia kupata nafasi ya kuwa Mgeni mahususi katika kutembelea mabamba mbalimbali yaliyoko katika Maonyesho hayo, ambapo amesema Maonyesho yameandaliwa vizuri na washiriki ni wengi linatia hamasa, hususani ushiriki wa bidhaa mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi limeongezeka, pia pia kuongezewa Kwa makampuni ya Madini hasa wanaonyesha Teknolojia ya Madini.

" Lakini pia kwa mara ya kwanza Maonyesho hayo yameleta Watanzania wanaochimba Madini kutoka Mikoa mbalimbali kuja Tanzania, hivyo niwapongeze sana wandaaji Kwa jambo hili kumbwa na muhimu" amesema Mbunge Kanyasu.

Aidha amesema jambo pekee ambalo wananchi wanatakiwa kujua ni kwamba bado walengwa ( wachimbaji wenyewe ) ado hawajafikiwa  kiasi cha kutosha.

" Ziko Kampuni ambazo lazima wawafuate wachimbaji madogo kule chini, Maonyesho haya hawawalengi makampuni makubwa kama GGM, Bakrifu, na Sota Mining, yanalenga wachimbaji wadogo kwahiyo tuangalie namna ya kuwafuata wale wachimbaji wadogo kule chini hasa  kwenye kuwapeleka Teknolojia, mitaji, lakini kwenye kuwawekea bima " amefafanua Mbunge Kanyasu.

" Kwasababu mabosi wamekuja hapa,  lakini wale wachimbaji wenyewe wako kwenye mashimo, ambao hata hawajapata nafasi ya kuja  kuona Maonyesho haya licha ya kuwa wao ndio wahusika wakuu, na ndio wanaokufa kwa kuangukiwa na miamba" amesema Mbunge Kanyasu

Aidha amesema kadiri inavyoonekana  Geita ilivyo sasa sivyo ilivyokua zamani, kuanzia Kasama mpaka Geita amjini palikua na msitu Mkubwa sana, lakini  miti yote imekwisha kwasababu ya Uchimbaji wa madini ( Matumizi ya Matimba) 

" Sasa iko haja ya kutafuta Teknolojia itakayookoa Misitu itakayobaki ili tusiendelee kukata miti yote inayobaki tutaharibu hali ya hewa, kuna Uhusiano mkubwa wa hali ya hewa ya Kanda ya ziwa na Misitu ya asili iliyokuwepo, kwahiyo tuchimbe Madini tutengeneze pesa, zile pesa zirudi kupanda miti" amesema Mbunge Kanyasu.

" Kazi nzuri imefanywa na Wizara ya Maliasili na Utalii pale mbele ya Katolo ule msitu wa Bihalamulo wamepanda hekta 69,000 pale wamepanda msitu mkubwa, ifanyike hivyo kwenye maeneo yote yaliyokua na msitu wa asili lakini imevunwa kwenda kwenye madini kwaajili ya kufidia ile Misitu ambayo imeharibika, Mimi nafikiri kwakufanya hivyo tutaendelea kuwa salama zaidi Kwa hali hiyo" ameongeza.

Ameiomba Wizara ya madini kuhakikisha kwenye Maonyesho kama hayo mwakani, tuwe na Banda linaloonyesha bidhaa mbalimbali zilizokamili za mawe aina mbalimbali, maana tulipofanya Maonyesho ya Madini Dar es Salaam tulikua na watengenezaji  wa bidhaa mbalimbali kama mikufu, Mikanda, shanga, heleni, shanga, vitu vingi mbalimbali ambao waliletwa na Wizara.

Naye mfanyakazi wa Kampuni ya uchimbaji Madini ya Tanzanite kutoka Franone Mining & Gems Company Ltd Furaha  Mshai amesema ujio wao kwenye Maonyesho hayo ni fulsa pekee ya kutangaza Madini yao ya Tanzanite na kuwaonyesha Watanzania Madini  pekee yanayopatikana  hapa nchini ambayo ni  Tanzania na Dunia Kwa ujumla.

Mshai amesema  Madini hayo yamekua ni kivutio kikubwa katika Maonyesho hayo yamekua ni utajiri mkubwa wa nchi ya Tanzania

Tume ya Madini ije na Teknolojia ya kukamata Madini ya dhahabu, Shaba na mengine-Mbunge Kanyasu  Tume ya Madini ije na Teknolojia ya kukamata Madini ya dhahabu, Shaba na mengine-Mbunge Kanyasu Reviewed by VISIONMEDIA on September 28, 2023 Rating: 5

Post Comments

Powered by Blogger.