test

MWANACHUO ASHINDA MILIONI MOJA YA TIGO CHA WOTE

 Na Mwandishi Wetu. 

Ana Juma Mabibi , mwanachuo ni miongoni mwa washindi wa Milioni Moja ambayo itamsaidia  kutimiza  mahitaji yake muhimu ya chuo na kufanya vizuri zaidi katika masomo yake kutokana na Kampeni ya Tigo CHA WOTE  ambapo hadi leo Septemba , 01 , 2023 Tigo wameshatoa Fedha Taslim na zawadi mbalimbali kwa Washindi zaidi ya elfu 22,400 Nchi Nzima .



Akizungumza Leo Septemba , 01 , 2023. Wakati wa Kuwakabidhi Mfano wa Hundi Baadhi ya Washindi wa Milioni Moja Moja  waliobahatika kufika Tigo Makao Makuu, Meneja Wa Wateja Maalum Tigo Pesa Bi Mary Rutha amesema kuwa hadi sasa wameshapatikana washindi zaidi ya 22,400 kutoka maeneo mbalimbali nchini .
" Leo tunayo furaha kubwa kuwa na baadhi ya washindi wetu Kampeni  ya TIGO CHA WOTE ambao hawa ni washindi wa Milioni Moja Moja kila mmoja, Lakini niwakumbushe Watanzania kwamba kila siku CHA WOTE inatoa zawadi ikiwemo pesa taslimu hadi Milioni Moja kwa washindi 320 kila siku , kuibuka mshindi ni rahisi tu unachotakiwa ni kufanya miamala na Tigo Pesa kama Kutumia Lipa Kwa Simu , Kununua Vifurushi , Kulipia Bili kwa Tigo Pesa , n.k kwa kufanya ivyo nawewe siku si nyingi utakua miongoni mwa Washindi wa Kampeni hii ya CHA WOTE ".  maana bado washindi zaidi ya elfu 10 wanatafutwa" Alisema Bi. Mary Rutha 

Mshindi mwingine ni Abdurazaq Mohammed muuza LAPTOP ambaye amesema ushindi huo utamsaidia kuongeza baadhi ya Vifaa vyake vya dukani kama vile simu , Laptop na baadhi ya ADAPTOR .



MWANACHUO ASHINDA MILIONI MOJA YA TIGO CHA WOTE MWANACHUO ASHINDA MILIONI MOJA YA TIGO CHA WOTE Reviewed by Adery Masta on September 01, 2023 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.