test

WAZIRI wa Madini Antony Mavunde amempongeza mwekezaji mzawa wa Kampuni ya Blue Coast Athanasi Inyasi kwa Uwekezaji wake unaochangi kutoa ajira 360 Kwa jamii.

Na Mary Margwe, Geita





Hayo amebainisha Jana wakati akizungumza mbele ya mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Geita Martin Shigela, wakati  alipomtembelea mmoja kati ya wawekezaji wazawa katika mkoa huo Athanas Inyasi.


Mavunde amesema uwepo wa sheria hiyo umewanufaisha na unaendelea kuwanufaisha wawekezaji walioamua kuwekeza hapa nchini.


Aidha amesema anahitaji kuonanwazee wengi na wawekezaji kama Mzee Inyasi na kuonesha kufurahishwa na kuridhishwa na uwekekzaji unaofanywa na Mwekezaji huyo na kutumia nafasi hiyo kuwataka wananchi wengine kuhakikisha wanajikita zaidi katika kuwekezaji kwenye sekta mbalimbali hapa nchini


Serikali  ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Dkt Samia Suluhu Hassan itaendelea kusimamia sheria hii  ili kuhakikisha watanzania wanaendelea kunufaika na rasilimali zao zikiwemo  za  sekta ya madini.


Aidha amesema Serikali ya awamu ya sita imeboresha mazingira ili wawekezaji wengi zaidi wakiwemo wazawa kuhakikisha  wanafanya uwekezaji, hivyo anahitaji kuwaona akina Mzee Inyasi wengi.


" Tunahitaji kuwaona  akina mzee Inyasi wengi zaidi na  mwisho wa siku tuweze kuyaona matokeo ya uchumi wa madini  katika maisha ya watanzania,  na  mwisho wa siku tuweze kuyaona matokeo ya uchumi wa madini  katika maisha ya watanzania .”amesisitiza Mavunde


 Naye Mwenyekiti wa Makampuni ya Blue Coast Athanas Inyasi amesema sheria ya local Contect imesaidia kwa kiasi kikubwa kutokana na kuleta mafanikio makubwa kwa watanzania,huku ajira 360 zikiwa zimetolewa na kampuni hiyo.


Ametumia nafasi hiyo kumshukuru Rais Dkt  Samia Suluhu Hassan kuboresha mazingira ya uwekezaji huku akiahidi kuendelea kufanya uwekezaji wenye tija kwa maslahi ya jamais na Taifa kwa ujumla.


Awali akitoa taarifa ya mradi huo Mkurugenzi Mtendaji wa Blue Coast  Ndahilo Athanas amesema kampuni hiyo pamoja na mambo mengine Pia imekuwa ikichangia katika shughuli za Maendeleo ambapo mpaka sasa wameshajenga  miundombinu ya madarasa na kununua madawati kwa shule za msingi Nyamalembo na Mseto zilizopo katika mkoa wa Geita.


Aidha amesema kampuni imekuwa ikilipa kodi kwa weledi na hivyo kupata tuzo ya mlipaji bora wa kodi na hatimaye kuwekwa kwenye kundi la walipa kodi wakubwa.


" Kampuni yetu ninya kizawa na inajishughulisha na usafirishaji na usambazaji wa bidhaa na mizigo ya aina zote  Kwa zaidi ya miaka 20 ndani na nje ya nchi kama afrika Mashariki na kati, pamoja na nchi zamkusini mwa afrika" amesema Athanasi.

WAZIRI wa Madini Antony Mavunde amempongeza mwekezaji mzawa wa Kampuni ya Blue Coast Athanasi Inyasi kwa Uwekezaji wake unaochangi kutoa ajira 360 Kwa jamii. WAZIRI wa Madini  Antony Mavunde amempongeza mwekezaji mzawa wa Kampuni ya Blue Coast Athanasi Inyasi kwa Uwekezaji wake unaochangi  kutoa ajira 360 Kwa jamii. Reviewed by VISIONMEDIA on September 28, 2023 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.