test

Gekul Apeta Tena! Shauri la Jinai


 Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Manyara kwa mara nyingine imetupilia mbali Shauri la rufaa ya jinai namba 577 la mwaka 2024 iliyokuwa inamuhusu Hashimu Ally ambaye ni mrufani dhidi ya Pauline Gekul ambaye alikuwa ni mrufaniwa.


Mahakama hiyo imeitiishwa kwa ajili ya kutoa uamuzi wa mapingamizi na sababu za rufaa ambazo awali ziliwasilishwa na kusikiliza Mahakamani.


Hayo yamebainishwa Leo April 15, 2024 mbele ya Jaji Devotha Kamuzora, aliyesikiliza rufaa hiyo namba 577/2024 ambapo katika rufaa hiyo Ally anapinga uamuzi uliofanywa na Mahakama ya Wilaya ya Babati Desemba 27, 2023 ya kuiondoa kesi hiyo mahakamani baada ya Mkurugenzi wa Mashitaka Nchini (DPP) kutokuwa na nia ya kuendelea na kesi hiyo.


#visionmediatz

Gekul Apeta Tena! Shauri la Jinai Gekul Apeta Tena! Shauri la Jinai Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on April 15, 2024 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.