test

ASKOFU AJINYONGA CHANZO KIKIWA NI MADENI.

 



Askofu Mkuu wa Makanisa ya Methodist, Joseph Bundala amejinyonga ofisini KWAKE kwa kutumia waya wa simu buku akieleza chanzo ni  madeni yaliyokuwa yanamkabili.


Tukio Hilo lilitokea mei 16 saa moja usiku kwenye choo Cha ofisi yake iliyoko ndani ya kanisa la Methodist,meriwa jijini Dodoma.


Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Alchelaus Mutalemwa amesema Jana mei 17 2024 kuwa jeshi la polisi linachunguza tukio Hilo.


Uchunguzi katika eneo la tukio umekuta ujumbe unaeleza sababu za kujinyonga ni madeni na mgogoro uliopo katika uendeshaji wa shule binafsi.


Mwenyekiti wa mtaa wa meriwa ,Gervas Lugunyale amesema juzi saa moja usiku alipigiwa simu na mmoja wa wachungaji wa kanisa Hilo akiomba aende akawasaidie kwani wamemkuta Askofu Bundala (55) akiwa amejinyonga ndani ya ofisi.


"Nilipofika nikapiga simu kwa watu wa usalama  Ili waje kutusaidia lakini nikaingia ndani ofisini,bahati mbaya nilikuta Baba Askofu ameshajichukulia maamuzi mikononi amejinyonga,ameshafariki Dunia , alisema 


Amesema kwenye meza iliyokuwa ofisini kwake Askofu huyo walikuta waraka ambao kwa kifupi ulikua umeandika Madeni anayodai na anayodaiwa.


Amesema polisi walikwenda kuchukua mwili na kuupeleka kuuhifadhi ," ni tukio la ajabu kubwa linaumiza kwa sababu huyu ni Askofu wa Tanzania ambaye watu wengi wanamwamini na wanamjua inaonekana hukuwa na watu wa kuwaambia haya yaliyomsibu angepata watu wa kumshauri"alisema 


Amesema Mchungaji wa kanisa Hilo ambaye hakumtaja jina alimweleza kuwa aliagizwa na Askofu kwenda dukani kumnunulia biscuits na soda kabla ya kwenda kwenye kipindi Cha Maombi eneo la makole, jijini Dodoma.


"Alifanya hivyo na kwenda makole kwenye kipindi akamuacha peke yake akidhani anaendelea kuratibu kazi zake za uaskofu lakini aliporudi saa moja usiku Giza likiwa limeshaingia ,alishtuka kuona mlango wa ofisi ukiwa wazi na ndani Kuna Giza , alisema Mwenyekiti huyo.


Amesema Mchungaji huyo alimweleza kuwa alishtuka kuona Hadi muda huo mlango ukiwa wazi na kwamba alimuacha Askofu akiwa ndani jambo lililomfanya aingie ndani ya ofisi.


Amesema alipoingia kwenye kiti hakuona mtu ila alipokwenda kwenye choo Cha ofisi ya Askofu alikuta shuka lakimasai akidai huenda alitaka kutumia kujinyonga.


Alieleza,"inaonekana alitumia waya wa simu kufunga kwenye Sirisha akajinyonga siku zote ,siku zote ukiwa na jambo shirikisha wenzako ,rafiki, ndugu zako ,walimu,wazee waambie changamoto zako ukiwaambia unaweza kupata ushauri ukaokoa maisha yako",Alisema


BAADHI YA VIONGOZI WA DINI MBALIMBALI 

"Askofu Mkuu wa kanisa la pentecoste Bible fellowship Church in Tanzania ( Jafeth Mapogo amesema Kila kanisa lina utaratibu wake wa kuwazika  viongozi wao wa dini hivyo aliitaka jamii iwaache Ili wafuate waliyojiwekea


Askofu Mapogo amesema Kila dini inajua kuua ni dhambi na alichokifanya Askofu huyo ni kujihukumu kwa kukatisha uhai wake,yapo baadhi ya makanisa ambayo hayatoi huduma Kwa mtu aliyejiua.


Amesema amefanya hivyo kama binadamu na kuwataka watu kutoingilia majukumu ya Mungu ya KUHUKUMU Bali wamwachie mwenyewe aliyempa Wito wa kuwa Askofu.


"Ila anastahili kuzikwa kama Ilivyo binadamu yeyote anayemaliza mwendo wake awe na dini au asiwe nayo awe Askofu au muumini asiye na cheo ni lazima azikwe kwa heshima zote kwa sababu anastahili" alisema




ASKOFU AJINYONGA CHANZO KIKIWA NI MADENI. ASKOFU AJINYONGA CHANZO KIKIWA NI MADENI. Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on May 18, 2024 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.