test

SOMA HAPA : JINSI YA KUJIPATIA GB 1 BURE KWA KUPAKUA SUPER APP YA TIGO PESA

  Na Mwandishi Wetu

Kadili siku zinavyozidi kusonga ndivyo teknolojia nayo inavyozidi kushika kasi na hapo ndipo Kampuni ya mtandao wa simu ya Tigo ilipoamua kuja kidijitali zaidi kwa kuzindua App ya kisasa kabisa ‘Super App’ ya Tigo Pesa ambayo itawarahisishia maisha watumiaji wa huduma za kampuni hiyo.

Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Afisa Mkuu wa Tigo Pesa, Angelica Pesha amesema App hiyo imekuja kufanya mapinduzi makubwa ya kuwarahisishia na kuwaboreshea maisha watumiaji wa mtandao huo kwa kutumia App hiyo mpya.

Angelica amesema kampuni hiyo ndiyo iliyoanza kuja na App ya kufanya miamala ya Tigo Pesa miaka kumi iliyopita lakini pamoja na mafanikio ya App hiyo wameonelea waje na App yenye ubora zaidi inayoendana na kipindi hiki ukilinganisha na ile ya miaka kumi iliyopita.

Ameendelea kusema baadhi ya vitu vilivyoboreshwa kwenye App hiyo ni pamoja na kuweza kufanya miamala kwa watu watatu kwa pamoja jambo ambalo awali halikuwepo, kununua vifurushi kirahisi zaidi, kufanya malipo mbalimbali na mengineyo.

App hiyo amesema ina kasi zaidi na ni rahisi kutumia ambapo inapatikana kwa watumiaji wote wa Smart Phone na Smart Kitochi.

Wateja wote watakaoipakuwa na kuanza kuitumia hiyo watapewa ofa ya GB 1 ya bure.  Ama kweli Tigo yajayo yanafurahisha.

SOMA HAPA : JINSI YA KUJIPATIA GB 1 BURE KWA KUPAKUA SUPER APP YA TIGO PESA SOMA HAPA : JINSI YA KUJIPATIA GB 1 BURE KWA KUPAKUA SUPER APP YA TIGO PESA Reviewed by Adery Masta on May 17, 2024 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.