Mashindano ya *DK SAMIA AND GEKUL* yamehitimishwa rasmi kwa kucheza fainali katika uwanja wa Darajani November 10
Ambapo timu zilizofika fainali kwa Kundi la timu za Kata ni Kata ya *SIGINO* na *BAGARA* ambapo Kata ya *BAGARA* ikiibuka mshindi kwa magoli mawili
Huku kundi la timu za taasisi zilizofika fainali ni Timu ya *BAJAJI na EAGLE* ambapo timu ya Eagle ilibuika mshindi kwa magoli sita
Washindi wa Tim hizo zote mbili kilaa moja ameondoka na Milioni moja huku washindi wa pili wakiondoka na laki Tano na kufanya jumla zawadi zilizotolewa kuwa Milioni tatu *Tsh 3,000,000*
Akihitimisha michuano hiyo Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini Mheshimiwa *PAULINE GEKUL* ambaye ndiye alikuwa muasisi wa mashindano hayo ambayo awali aligawa mipira kwenye mitaa 35, Vijiji 13 Kata 8 na Taasisi 27 zilizokadiriwa kuwa thamani ya zaidi ya Million ishirini *20,000,000* huku Gharama za uendeshaji wa Ligi hiyo zikiwa zaidi ya Million kumi Tsh *10,000,000* hivyo kufanya Jumla ya Gharama zote kufika zaidi ya Million thelathini na tatu *Tsh 33,000,000*
Ametumia nafasi hiyo kuzipongeza timu zote kwa kufika hatua ya Fainali huku akisema wachezaji waliopatikana wapatao 40 kutoka kwenye timu zote zilizoshiriki watatafutiwa kocha ili kuwaendeleza na kuwa na Timu ya Jimbo
Akitoa salamu za chama Cha Mapinduzi Katibu wa Chama hicho Wilaya ya Babati Mjini Ndug *MOHAMED CHOLLAJE* amempongeza Mbunge huyo kwa kutekeleza ilani ya Chama hicho kwa vitendo
Kwa upande wa Chama Cha mpira wa Miguu Wilaya ya Babati ambao wamepewa Jukumu ya kuwa walezi wa timu ya Jimbo wameahidi kuendeleza kile alichokianzisha Mheshimiwa Mbunge
MASHINDANO YA DK SAMIA& GEKUL CUP YAHITIMISHWA BABATI MJINI.
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
November 11, 2024
Rating:
No comments: