test

PSSSF YAWAPA MBINU WASTAAFU WATARAJIWA JIJINI MBEYA JINSI YA KUISHI NJE YA UTUMISHI WA UMMA

 Na Mwandishi Wetu.

MFUKO wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) umekutana na wanachama wake wa mkoa wa Mbeya wanaotarajia kustaafu hivi karibuni na kuwapa mafunzo (mbinu) bora ya kuishi baada ya kustaafu utumishi wa umma.

                      

Akiwapa mbinu hizo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa PSSSF, Meneja wa Pensheni za Wastaafu, Bw. Kwame Temu, amewaambia kuwa ni busara mara mstaafu atakapopokea Mafao yake, awekeze katika viwanda vidogo vidogo na vya kati, uwekezaji katika masoko ya fedha, kilimo biashara na ujasiriamali kwa ujumla.

                                 

“Mafao ya uzeeni yanayolipwa kwa wastaafu yakitumika vizuri yanaweza kutoa mchango katika kuendeleza miradi mbalimbali, kutengeneza ajira kwa vijana, kuongeza pato la mstaafu na hatimaye pato la Taifa.” Amesema Bw. Temu.

Aidha mgeni rasmi katika mafunzo hayo, Mkuu wa Wilaya ya Mbeya mjini, Mhe. Benno Malisa, yeye amewaasa kuzingatia mafunzo hayo.

“"Kati ya zawadi ambayo PSSSF imewapa wastaafu ni mafunzo haya, tuwashukuru sana, tutumie fursa hii kusikiliza kwa makini mafunzo mnayopewa na PSSSF pamoja na elimu inayotolewa na wadau wa sekta za fedha ili fedha zenu muwekeze sehemu sahihi na salama msije kumbana na matapeli.” Aliasa

Aidha amewaonya kujihadhari na washaru watakaoibuka katika kipindi hiki ambacho wanajua kuwa wastaafu watapokea malipo.

“Watu wanajua sasahivi kuna pesa mtapata hivyo washauri watakua wengi, mjiepushe nao," Alionya.












PSSSF YAWAPA MBINU WASTAAFU WATARAJIWA JIJINI MBEYA JINSI YA KUISHI NJE YA UTUMISHI WA UMMA  PSSSF YAWAPA MBINU WASTAAFU WATARAJIWA JIJINI MBEYA JINSI YA KUISHI NJE YA UTUMISHI WA UMMA Reviewed by Adery Masta on November 12, 2024 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.