test

JE UNA MATATIZO YA MACHO ? YAS TANZANIA NA BILALI MISSION WAJA NA HUDUMA BURE MKURANGA

  Na Mwandishi Wetu.

                             

Mkuranga, Pwani – Taasisi ya Bilali Mission Tanzania kwa kushirikiana na Kampuni ya Yas Tanzania wamefanikisha zoezi la utoaji wa huduma za matibabu ya macho kwa wakazi wa Mkuranga, mkoani Pwani. Zoezi hilo limewaleta pamoja wananchi wengi waliopata fursa ya kupimwa macho na kupatiwa matibabu bila gharama.

                               

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua huduma hizo, Mkurugenzi wa Yas Dar Es Salaam na Pwani , Aidan Komba, alisema:

"Kusogeza huduma za afya ya macho kwa jamii ni sehemu ya dhamira yetu ya kusaidia kuimarisha afya ya Watanzania. Tunafurahi kuona ushirikiano wetu na Bilali Mission Tanzania ukiwanufaisha wananchi wa Mkuranga."

                          

Waziri wa Mifugo na Uvuvi, ambaye pia ni Mbunge wa Mkuranga, Mhe. Abdallah H. Ulega, aliwashukuru waandaaji kwa juhudi zao na kuwapongeza wananchi kwa kujitokeza kwa wingi.

"Huduma hizi ni muhimu sana kwa wananchi wetu, nawashukuru Yas Tanzania na Bilali Mission kwa kuhakikisha wananchi wa Mkuranga wanapata matibabu haya muhimu. Serikali itaendelea kushirikiana na wadau kama hawa ili kuboresha maisha ya wananchi wetu," alisema Mhe. Ulega.

Zoezi hilo limeonekana kuwa msaada mkubwa kwa wakazi wa Mkuranga, huku likitarajiwa kuimarisha afya ya macho na kuongeza ufanisi wa maisha ya kila siku.


Mkurugenzi wa Yas Dar Es Salaam , Aidan Komba, akishuhudia huduma za matibabu ya macho zinavyotolewa. Taasisi ya Bilali Mission Tanzania, kwa kushirikiana na Kampuni ya Yas Tanzania, wameendesha zoezi la utoaji wa huduma za afya ya macho kwa wakazi wa Mkuranga, mkoani Pwani.

Mhe. Abdallah H. Ulega, Waziri wa Mifugo na Uvuvi na Mbunge wa Jimbo la  Mkuranga, akiwasalimu wananchi wa jimbo lake waliojitokeza kupata huduma za matibabu ya macho katika zoezi lililoendeshwa kwa ushirikiano kati ya Taasisi ya Bilali Mission Tanzania na Kampuni ya Yas Tanzania.


                                  

                                    

JE UNA MATATIZO YA MACHO ? YAS TANZANIA NA BILALI MISSION WAJA NA HUDUMA BURE MKURANGA JE UNA MATATIZO YA MACHO ? YAS TANZANIA NA BILALI MISSION WAJA NA HUDUMA BURE MKURANGA Reviewed by Adery Masta on December 07, 2024 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.