test

MATUKIO YA UKATILI YAPUNGUA KWA MKOA WA MWANZA 2024

 Takwimu za Matukio ya kikatili yamepungua kwa Mkoa kwa Mkoa wa Mwaka 2024 ukilinganisha na mwaka 2023,



Akizungumza katika Maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili kamanda wa polisi Mkoa wa Mwanza Naibu kamishna wa Polisi Wilbroad Mutafungwa Amesema kuwa Matukio hayo yamepungua kutoka 1140Mwaka2023 Mpaka 118 kwa Mwaka 2023 Huku Matukio 22 ya ukatili kwa Watoto yamepungua.



Kamanda Mutafungwa amesema kuwa Changamoto kubwa inayowakabili ni Usuluhishi wa kesi unaofanywa Nyumbani baada ya makosa kufanyika.

Naye mgeni Rasmi katika Maadhimisho hayo Mkuu wa wilaya ya Nyamagana Bi,.Amina Makilagi ameeleza kuwa Serikali ina Mikakati kabambe ya kupambana na Ukatili Huku akiisihi Jamii kuungana na kutoa Ushirikiano kwa vyombo vya Ulinzi na usalama Katika kutoa Taarifa za Ukatili.






Nao viongozi Mbali mbali wa Dini Taasisi wameungana na Serikali katika kupinga Matukio hayo ambayo yamekuwa Tishio kubwa kwa Jamii.

Kwa Upande wao Wananchi wameeleza kuwa Takwimu za Ukatili zimeshuka lakini Matukio Mengi ya Ukatili yamekuwa hayaripotiwi Kutokana na sababu za Kulindana, Hivyo kuisihi Jamii kutofumbia Macho Matukio hayo ili kutokomeza Matukio hayo.

MATUKIO YA UKATILI YAPUNGUA KWA MKOA WA MWANZA 2024 MATUKIO YA UKATILI YAPUNGUA KWA MKOA WA MWANZA 2024 Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on December 11, 2024 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.