test

YAS WASHINDA TUZO YA MTANDAO WENYE KASI ZAIDI YA INTANETI KUTOKA OOKLA KWA MARA YA PILI MFULULIZO

 Na Mwandishi Wetu

 Kampuni ya Mawasiliano ya YAS TANZANIA @yastanzania_  imeshinda Tuzo ya kuwa kampuni namba moja ya Mawasiliano yenye mtandao wa Internet wenye kasi zaidi "OOKLA SPEEDTEST AWARD FOR THE FASTEST MOBILE NETWORK IN TANZANIA" ambapo kampuni ya YAS imeibuka mshindi wa kwanza kwa mwaka 2024 nakuziacha mbali kampuni zingine zinazotowa huduma ya mawasiliano nchini.

                              

Akitangaza ushindi huo wa YAS TANZANIA hii leo Jijini Dar es Salaam, Kaimu CEO wa kampuni ya YAS Tanzania, Bwana JEROME ALBOU amesema wamekuwa washindi wa tuzo hiyo kwa Mwaka wa pili mfululizo na kwamba Yas Tanzania imepiga hatua kubwa sana kwenye kutoa huduma ya Internet yenye kasi zaidi nchini hivyo kukidhi vigezo vya kikataifa

                             

Aidha JEROME ALBOU amesema Kampuni ya YAS TANZANIA Imewekeza Jumala ya Trioni 1 za kitanzania katika kuhakikisha Tanzania bara na Tanzania Visiwani  inakuwa na minara 4000 ya kiwango cha 4G huku wakiifikidha 5G kwenye miji yote mikubwa Tanzania 

                             

"YAS Tanzania imedhamiria kubadilisha sekta ya Mawasiliano kwakuwapa wateja wake huduma zakisasa za Kiteknolojia zinazohitajika sokoni kwalengo la kukuza biashara, kuleta usawa na upatikanaji wa huduma jumuishi, ubunifu katika Teknolojia na hivyo kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa nchi" Amesema Jerome 

CEO JEROME ALBOU, Ameongeza kuwa wanapo sherehekea ushindi huu wa Tuzo kutoka OKLA bado wanazingatia jukumu lao la kutoa huduma bora katika sekta ya Teknolojia ya Mawasiliano nchini,  nakwamba wamejiwekea malengo madhubuti ya kuongeza wigo wa upatikanaji wa Mtandao imara na kuleta mapinduzi katika sekta ya Digitali.

Akiwasilisha Ripoti ya ushindi wa YAS TANZANIA, OSAMA NAWAYSE kutoka Ookla amesema, kampuni ya Yas Tanzania imeshinda kwa asilimia 68.81 kwakuwa na Internet yenye kasi zaidi na hakuna kampuni yoyoye ya Mawasiliano Tanzania imefikia kiwango hicho.

Kwa upande wa Medium dowloder speed YAS TANZANIA imepata asilimia 43 ikizitangulia kampuni zote za Mawasiliano nchini Tanzania sambamba na kuongoza katika vipengele vingine tofauti tofauti kuusiana na masuala ya upatikanaji wa Internet yenye kasi zaidi nchini Tanzania.











YAS WASHINDA TUZO YA MTANDAO WENYE KASI ZAIDI YA INTANETI KUTOKA OOKLA KWA MARA YA PILI MFULULIZO YAS WASHINDA TUZO YA MTANDAO WENYE KASI ZAIDI YA INTANETI KUTOKA OOKLA KWA MARA YA PILI MFULULIZO Reviewed by Adery Masta on December 10, 2024 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.