test

POLISI KILIMANJARO YAFANYA OPERESHENI KALI STENDI KUU YA MABASI

 


 Jeshi la polisi kupitia kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Kilimanjaro limewataka madereva, wamiliki wa mabasi pamoja na abiria kutoa ushirikiano katika kulinda usalama wao kwa mujibu wa sheria na taratibu zilizowekwa na taasisi na mamlaka ya serikali ili kuepusha ajali.



Hayo yamesemwa na kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro SACP Simon Maigwa katika ukaguzi wa mabasi yaendayo mikoani kupitia kampeni ya abiria paza sauti katika stendi kuu ya mabasi mjini Moshi.



Ukaguzi huo wa vyombo vya usafiri wamepima ulevi madereva kama moja ya mikakati ya kuzuia ajali barabara kutokana na baadhi ya madereva kuhusishwa na matumizi ya vilevi kabla ya kuanza safari.


Awali akizungumzia lengo la ukaguzi huo Mkuu wa kitengo cha usalama barabarani mkoa wa Kilimanjaro SSP. Yusuph Kamota alisema ukaguzi huo unaenda sambamba na muendelezo wa kampeni ya kupunguza ajali za barabarani hasa kuelekea kipindi hiki Cha mwisho wa mwaka.


Naye afisa mfawidhi wa mamlaka ya usafiri wa ardhini Paul Nyello amesisiatiza suala la madereva kuzingatia Sheria za barabarani ili kulinda maisha ya wananchi.


Mwisho.

POLISI KILIMANJARO YAFANYA OPERESHENI KALI STENDI KUU YA MABASI POLISI KILIMANJARO YAFANYA OPERESHENI KALI STENDI KUU YA MABASI Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on December 13, 2024 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.