WACHOMA JENEZA,KWA KUDAI KIFO KINA UTATA

test

Katika hali isiyokuwa ya kawaida baadhi ya vijana katika kijiji cha Kilanji kata ya Kipagalo wilayani Makete mkoani Njombe wamechoma moto jeneza lililokuwa limebeba mwili wa marehemu Kashinde Sanga (28) aliyefariki dunia jijini Dar es Salaam alikokuwa akifanya kazi dukani kwa madai kwamba kifo chake kina utata



Tukio hilo limetokea Aprili 9,2025 ambapo Vijana hao wameamua kuchangishana fedha za kutengeneza jeneza lingine ambalo wamelitumia kuuzika mwili wa marehemu na lile lililotoka na mwili Dar es Salaam likateketezwa kwa moto huku wakidai wamechoka vijana wao wanaokwenda kufanya kazi mijini kurudi wakiwa wamefariki dunia wakidai tukio kama hilo si la kwanza kutokea kijijini hapo katika siku za hivi karibuni


Mwenyekiti wa kijiji cha Kilanji Erasto Sanga akizungumza nasi amekiri kutokea kwa tukio hilo na kudai kuwa kiongozi wa waliokuja na mwili wa marehemu amesema kijana huyo aligundulika kufariki dunia asubuhi wakati kijana mwenzake aliyekuwa akilala naye kumuamsha ajiandae ili waende kazini na kugundua mwenzake amefariki jambo ambalo limeibua utata kwa familia na baadhi ya waombolezaji wakiwemo vijana hao


Mmoja wa waombolezaji kijana Agrey Mbwilo amesema kwa sasa hawako tayari kukubali watoto wao kuchukuliwa kwenda mijini kuajiriwa kufanya kazi iwe biashara au kazi za  ndani na badala yake watajikita kuwasomesha ili wajikwamue kiuchumi na hata kujiajiri kupitia kilimo kijijini hapo.


#edmotvupdates #edwinmoshiupdates

WACHOMA JENEZA,KWA KUDAI KIFO KINA UTATA WACHOMA JENEZA,KWA KUDAI KIFO KINA UTATA Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on April 10, 2025 Rating: 5

Post Comments

Powered by Blogger.