test

WAUAJI WA MWANACHUO WAUAWA MBEYA

 Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya limesema watuhumiwa watatu wa mauaji ya mwanachuo Shyrose Mabula wamefariki dunia katika matukio tofauti wakiwa wanawakimbia askari, huku msako wa kuwasaka watuhumiwa wengine ukiendelea, akiwemo mganga wa kienyeji.



Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Benjamin Kuzaga, watuhumiwa wawili waliotambulika kwa majina ya Websta William Mwantebele na Edward Christopher Kayuni walipigwa risasi miguuni na askari walipojaribu kutoroka. Hata hivyo, walipofikishwa hospitalini ilibainika kuwa walishafariki dunia.


Kamanda Kuzaga ameongeza kuwa mtuhumiwa mwingine, Marwa Nyahega John, amefariki dunia baada ya kujirusha kutoka kwenye gari la polisi na kupata jeraha kubwa kichwani.


Tukio hilo limetokea wakati askari walipokuwa wakimsindikiza kwenda kwa mganga wa kienyeji katika eneo la Isyesye jijini Mbeya, ambako alidai kupeleka kidole na nguo ya ndani ya marehemu kwa ajili ya kufanyiwa zindiko ili wasikamatwe na polisi.

WAUAJI WA MWANACHUO WAUAWA MBEYA WAUAJI WA MWANACHUO WAUAWA MBEYA Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on September 29, 2025 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.