Mbunge wa Jimbo la Tunduru Kaskazini Ndugu Ado Shaibu amechangia Shilingi Milioni tatu katika harambee ya ujenzi wa Bwalo la Chakula na Ofisi ya Utawala katika Shule ya Msingi Jamhuri iliyopo Wilayani Tunduru.
Ndugu Ado ametoa mchango huo kwenye harambee ya wazazi iliyofanyika shuleni hapo leo tarehe 13 Desemba 2025 ambapo yeye alikuwa mgeni rasmi. Jumla ya Tsh. Milioni Sita na vifaa mbalimbali kama vile Simenti, mchanga na kokoto vilichangwa.
Shule ya Jamhuri imeshika nafasi ya pili kwa ufaulu katika Wilaya ya Tunduru na ya kwanza katika Jimbo la Tunduru Kaskazini katika Matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Darasa la Saba. Ndugu Ado amekubali ombi la uongozi wa shule hiyo kuwa mlezi wake katika kukabiliana na changamoto zake ili itimize lengo lake la kuongeza ziadi ufaulu.
Katika hotuba yake, Ndugu Ado amewapongeza wazazi na wadau waliochangia kwa harambee hiyo na kuahidi kuwa harambee hiyo itakuwa endelevu ili kuhakikisha ujenzi huo unakamilika. Ndugu Ado ameahidi kuwashirikisha wadau mbalimbali wa maendeleo ndani na nje ya Tunduru ili kuichangia zaidi shule ya Jamhuri.
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
December 13, 2025
Rating:



No comments: