test

KAULI YA KWANZA BARAZANI!

 


Kikao cha kwanza katika Baraza la Madiwani huwa hakina ajenda nyingi zaidi ya kuapisha madiwani, kuchagua Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri, Kuteua Kamati za Halmashauri na kupokea taarifa ya masuala yaliyofanyiwa kazi na Kamati ya Wakuu wa Idara (CMT) katika kipindi ambacho Baraza la Madiwani limevunjwa.



Kauli yangu ya kwanza katika Baraza la Madiwani Tunduru ilikuwa swali kwa Mwenyekiti  wa Halmashauri Ndugu Seif Dauda kumtaka aeleze nafasi ya Halmashauri atayoiongoza katika kukabiliana na changamoto za migogoro ya wakulima na wafugaji na uharibifu unaofanywa na tembo. Hoja hizo mbili ni sehemu ya changamoto kuu zinazowakabili wananchi ambao wamenipa imani kubwa. Tutaendelea kuyafuatilia masuala hayo na mengine yanayoathiri maisha ya WanaTunduru ili wapate maendeleo.

KAULI YA KWANZA BARAZANI! KAULI YA KWANZA BARAZANI! Reviewed by VISION MEDIATZBLOG on December 14, 2025 Rating: 5

No comments:

Powered by Blogger.