Mkuu wa Wilaya ya Mbulu, Mhe. Michael John Semindu, Mbunge wa Mbulu Vijijini, Dkt. Emanuel Nuwas, pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu, Ndugu Abubakar Abdallah Kuuli, kwa kushirikiana na Kamati ya Usalama ya Wilaya, wamefanya ziara katika Hospitali ya Kilutheri ya Haydom kwa lengo la kujionea utoaji wa huduma za afya.
Katika ziara hiyo, viongozi hao walijionea huduma mbalimbali zinazotolewa na hospitali kwa wananchi wa Wilaya ya Mbulu na maeneo jirani, pamoja na juhudi za uongozi na watumishi katika kuhakikisha huduma bora na salama zinawafikia wananchi. Pia walisisitiza umuhimu wa kuendelea kushirikiana ili kuimarisha zaidi sekta ya afya kwa manufaa ya jamii.
DC MBULU MBUGE , DED MBULU DC NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WATEMBELEA HYDOM HOSPITALI
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
February 24, 2026
Rating:
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
February 24, 2026
Rating:



No comments: