Na Mwandishi Wetu.
Mbunge wa Jimbo la Mbulu vijijini Dr Emmanuel NUWAS pamoja na viongozi WA HALMASHAURI ya Wilaya ya mbulu
Wamefanya mwendelezo wa ziara ya kusikiliza na kutatua kero za stendi, ambapo kwa mara ya mwisho Mheshimiwa aliahidi kuwaleta Mkuu wa Wilaya na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri.
Katika ziara hii, viongozi hao walifika na kukagua: Hali ya uchafu katika stendi mpya, Miundombinu ya stendi na Changamoto ya stendi ndogo ndogo nyingi zinazopunguza makusanyo ya mapato
Ikumbukwe kuwa hivi karibuni Mheshimiwa alitembelea stendi ya Haydom, akakutana na wananchi na viongozi kujadili changamoto hizi. Ziara ya leo ni uthibitisho wa dhamira ya dhati ya kushirikiana na mamlaka husika ili kuhakikisha suluhisho la kudumu linapatikana kwa ustawi wa wananchi.
DR NUWAS NA VIONGOZI WA HALMASHAURI MBULU DC WATEMBELEA STENDI YA HAYDOM
Reviewed by Adery Masta
on
February 23, 2026
Rating:
Reviewed by Adery Masta
on
February 23, 2026
Rating:




No comments: