Naibu waziri, ofisi ya rais – menejimenti ya utumishi wa umma na utawala bora, mhe. Regina Qwaray amesema serikali imeanzisha mfumo wa e-mrejesho ambao ni jumuishi unaomwezesha mwananchi kutuma,kufuatilia na kupokea mrejesho wa malalamiko,mapendekezo, maulizo au pongezi.
Amesema hayo leo katika kikao cha baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Babati, amesema mfumo huo utasaidia wananchi kutatuliwa changamoto zao kwa wakati.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Babati Emmanuela Kaganda , amesema changamoto zote ambazo zimeelezwa na madiwani zinafanyiwa kazi na kata zote zitafikiwa.
Aidha mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Babati John Noya, amewataka madiwani kusimamia miradi ya serikali kufuatia kuwepo kwa uharibifu wa miundombinu unaosababishwa na baadhi ya wananchi.
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
February 18, 2026
Rating:




No comments: