S/SGT wa Polisi Philomena Richard kutoka Kikosi cha Usalama Barabarani Polisi Msitu wa Tembo, Wilaya ya Simanjiro Mkoa wa Manyara akitoa elimu ya Umuhimu wa Abiria kufunga Mkanda wa Usalama ndani ya basi kwa abiria wanaofanya safari zao kupita Msitu wa Tembo Simanjiro
S/SGT Philomena amesema abiria kufunga mkanda si tu humlinda maisha yake ndani ya basi ila pia ni takwa la kisheria na kusema kuwa mkanda unaumuhimu sana pindi ajali inapotokea au gari kusimama ghafla
"ukifunga mkanda utakusaidia usitupwe nje au kugogana vibaya gari inapopata ajali au kusimama ghafla" amesema Philomena
Sasa ni muda sahihi kwa abiria na madereva wote kubadilika kwa kufunga mkanda wa usalama kabla ya kuanza safari ili kulinda Maisha
S/SGT Philomena Richard Akitoa Elimu ya Usala Barabara
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
February 04, 2026
Rating:
Reviewed by VISION MEDIATZBLOG
on
February 04, 2026
Rating:

No comments: